Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    5 / NURU INANGAA KATIKA UINGEREZA

    Mungu hakukubali Neno lake liharibiwe kabisa. Katika inchi mbalimbali za Ulaya watu waliosukumwa na Roho ya Mungu kwa kutafuta ukweli kama vile hazina zilizofichwa. Kwa bahati njema waliongozwa na Maandiko matakatifu, wakipendezwa kukubali nuru kwa bei yo yote itakayohitajiwa kwao wenyewe. Ingawa hawakuona vitu vyote wazi, walikuwa wakiwezeshwa kutambua mambo mengi ya ukweli yaliyozikwa ao fichwa tangu zamani.TSHM 30.1

    Wakati ulifika kwa Maandiko kupewa kwa watu katika lugha yao wenyewe. Dunia ilikwisha kupitisha usiku wake wa manane. Katika inchi nyingi kukaonekana dalili za mapambazuko.TSHM 30.2

    Katika karne ya kumi na ine “nyota ya asubuhi ya Matengenezo (Reformation)” ikatokea katika Uingereza. John Wycliffe alijulikana huko college kuwa mtu wa utawa wa elimu sana. Alielemishwa na hekima ya elimu, kanuni za kanisa, na sheria ya serkali, alitayarishwa kuingia katika kazi ngumu kubwa kwa ajili ya raia na uhuru wa dini. Alipata malezi ya elimu ya vyuo, na akafahamu maarifa ya watu wa mashule. Cheo na ukamilifu wa ufahamu wake viliamuru heshima za rafiki na maadui. Adui zake walizuiwa kutupa zarau juu ya chazo cha Matengenezo kwa kuonyesha ujinga ao uzaifu wa wale walioikubali.TSHM 30.3

    Wakati Wycliffe alipokuwa akingaliki huko college, akaingia majifunzo ya Maandiko matakatifu. Hata sasa Wicliffe alijifahamu kuwa mwenye hitaji kubwa, ambao hata mafundisho ya elimu yake wala mafundisho ya kanisa hayataweza kumtoshelea. Katika Neno la Mungu aliona kile ambacho alikuwa anatafuta bila mafanikio. Hapa akamuona Kristo akitangazwa kama mteteaji pekee wa mtu. Akakusudia kutangaza ukweli aliyovumbua.TSHM 30.4

    Kwa mwanzo wa kazi yake, Wycliffe hakujitia mwenyewe katika upinzani na Roma. Lakini kwa namna alivyotambua wazi zaidi, makosa ya kanisa la Roma, akazidi kwa bidii kufundisha mafundisho ya Biblia. Aliona kwamba Roma iliacha Neno la Mungu kwa ajili ya desturi za asili za watu. Akashitaki bila oga upadri kwa kuweza kuondoshea mbali Maandiko, na akataka kwa lazima kwamba Biblia irudishwe kwa watu na kwamba uwezo yake uwekwe tena ndani ya kanisa. Alikuwa mhubiri hodari na mwenye maneno ya kuamsha moyo, na maisha yake ya kila siku yalionyesha ukweli aliyohubiri. Ufahamu wake wa Maandiko, usafi wa maisha yake, na bidii yake na ukamilifu aliouhubiri yakampa heshima kwa wote. Wengi wakaona uovu katika Kanisa la Roma. Wakapokea kwa shangwe isiyofichwa kweli ambazo zililetwa waziwazi na Wycliffe. Lakini waongozi wa kiPapa wakajazwa na hasira: Mtengenezaji huyu alikuwa akipata mvuto mkubwa kuliko wao.TSHM 30.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents