Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Uvumilivu wa Mungu

    Karibu miaka makumi ine Bwana alikawisha hukumu zake. Kulikuwa kungali Wayahudi, wajinga ambao hawakujua tabia na kazi ya Kristo. Na watoto hawakufurahia nuru ambayo wazazi wao waliikataa kwa zarau katika mahubiri ya mitume, Mungu aliwezesha nuru kuangaza juu yao. Waliona namna gani unabii ulitimia, si katika kuzaliwa tu na maisha ya Kristo, bali katika kifo chake na ufufuo. Watoto hawakuhukumiwa kwa ajili ya zambi za wazazi; lakini wakati walipokataa nuru ingine waliopewa, wakawa washiriki wa zambi za wazazi na wakajaza kipimo cha uovu wao.TSHM 4.4

    Wayahudi katika ugumu wa mioyo yao wakakataa shauri la mwisho la rehema. Ndipo Mungu akaondoa ulinzi wake kwao. Taifa likaachwa kwa utawala wa mwongozi lililo mchagua. Shetani akaamsha tamaa kali sana na mbaya kuliko za roho. Watu wakakosa akili wakatawaliwa na nguvu na hasira ya upofu, ya shetani katika ukaidi wao. Marafiki na ndugu wakasalitiana wao kwa wao. Wazazi wakaua watoto wao, na watoto wazazi wao. Watawala hawakuwa na uwezo wa kujitawala wao wenyewe. Tamaa ikawafanya kuwa wajeuri. Wayahudi wakakubali ushuhuda wa uwongo kwa kuhukumu Mwana wa Mungu asiye na kosa. Sasa mashitaki ya uwongo yakafanya maisha yao kuwa si ya haki. Kuogopa Mungu hakukuwashitusha tena. Shetani alikuwa akiongoza taifa.TSHM 4.5

    Waongozi wa makundi ya upinzani wakaanguka mmoja juu za mwingine na kuwa bila huruma. Hata utakatifu wa hekalu haukuweza kuzuia ukali wao wa kutisha. Mahali patakatifu pakanajisiwa na miili ya waliouawa. Lakini washawishi wa kazi hii ya kishetani walitangaza kwamba hawakuwa na hofu yo yote kwamba Yerusalema ingeharibiwa! Ulikuwa mji wa Mungu. Hata wakati majeshi ya Waroma walipozunguka hekalu, makundi yalisimama imara kwa wazo kwamba Aliye juu angejitia kati kwa kushinda kwa maadui wao. Lakini Israeli alitupia mbali ulinzi wa Mungu, na sasa hakuwa na ulinzi.TSHM 5.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents