Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kosa Linasahihishwa

    “Basi wakati bwana arusi alipokawia, wao wote wakasinzia na kulala usingizi. Lakini saa sita ya usiku kulikuwa kelele: Tazama bwana arusi anakuja! tokeni kukutana naye.” Katika wakati wa jua kali wa mwaka 1844 ujumbe ukatangazwa katika maneno ya Maandiko kabisa.TSHM 190.6

    Kile kilichoongoza kwa maendeleo haya kilikuwa ni uvumbuzi kwamba amri ya Artasasta kwa ajili ya kurudishwa kwa Yerusalema, ambayo ilisaidia kujua mwanzo wa hesabu ya siku 2300, ikafanyika katika masika ya mwaka wa 457 B.C., na si kwa mwanzo wa mwaka, kama ilivyoaminiwa. Hesabu kutoka masika ya mwaka 457, miaka 2300 ikamalizika wakati wa masika ya mwaka 1844. Mifano ya Agano la Kale pia ilielekeza kwa wakati wa masika kama wakati ambao “kutakaswa kwa mahali patakatifu” kulipaswa kufanyika.TSHM 191.1

    Kuchinjwa kwa Kondoo wa Pasaka kulikuwa ni kivuli cha mauti ya Kristo, mfano ulitimilika, si kwa tukio tu, bali na kwa wakati. Kwa siku ya kumi na ine ya mwezi wa kwanza wa Wayuda, siku ile kabisa na mwezi ambapo kwa karne nyingi kondoo wa Pasaka alikuwa akichinjwa, Kristo akaanzisha karamu hiyo ambayo ilikuwa kwa kukumbuka mauti yake mwenyewe “Mwana-kondoo wa Mungu.” Kwa usiku uleule akakamatwa kwa kusulibiwa na kuuawa.TSHM 191.2

    Vivyo hivyo mifano ya kuelekea kwa kuja kwa mara ya pili inapaswa kutimizwa kwa wakati ulioonyeshwa katika kazi ya mfano. Kutakaswa kwa mahali patakatifu, ao Siku ya Upatanisho, kulitukia kwa siku ya kumi ya mwezi wa saba wa Wayuda wakati kuhani mkuu, alipokwisha kufanya upatanisho kwa ajili ya Israeli yote, na kwa hivyo akaondoa zambi zao kutoka kwa mahali patakatifu, akaja na kubariki watu. Kwa hiyo iliaminiwa kwamba Kristo angeonekana kuja kutakasa dunia kwa kuharibu zambi na wenye zambi, na kubariki watu wake wanaomungojea kwa kuwapa kutokufa. Siku ya kumi ya mwezi wa saba, Siku kuu ya Upatanisho, wakati wa kutakaswa kwa mahali patakatifu, ambao katika mwaka 1844 ulianguka kwa tarehe ya makumi mbili na mbili ya Oktoba, ilizaniwa kama ni wakati wa kuja kwa Bwana. Siku 2300 zingemalizika wakati wa masika, na mwisho ikaonekana kuwa wazi bila ubishi.TSHM 191.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents