Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Siku ya Bwana

    Asema nabii Isaya: ” Kwa siku ile mtu atatupa sanamu yake ya feza, na sanamu yake ya zahabu, walizojifanyizia kuziabudu, kwa panya na kwa popo; waingie katika mapango ya miamba, na ndani ya pahali pa juu ya mawe yaliyo pasukapasuka, toka mbele ya hofu ya Bwana, na toka utukufu wa mamlaka yake, wakati atakaposimama kutikisatikisa sana dunia”. Isaya 2:20, 21.TSHM 310.4

    Wale waliotoa vyote kwa ajili ya Kristo sasa wanakuwa katika salama. Mbele ya ulimwengu nausoni kwa mauti wameonyesha uaminifu wao kwake yeye aliyekufa kwa ajili yao. Nyuso zao, juzijuzi zilikuwa zenye kufifia na zenye kukonda, sasa zinangaa kwa ajabu. Sauti zao zinainuka kwa wimbo wa ushindi: “Mungu ni kimbilio letu na nguvu yetu, Msaada aliye karibu sana wakati wa mateso. Kwa hivi hatutaogopa, hata inchi ikibadilika, na hata milima ikihamishwa moyoni mwa bahari; Hata maji yao yakinguruma na kuchafuka, hata milima ikitikisika kwa kiburi chake”. Zaburi 46:1-3.TSHM 310.5

    Wakati maneno haya ya tumaini takatifu yanapopanda kwa Mungu, utukufu wa mji wa mbinguni unapita kwa milango inayofunguka kidogo. Ndipo pale panatokea kinyume cha mawingu mkono unaoshika mbao mbili za mawe. Sheria ile takatifu, iliyotangazwa kwa Sinai, imefunuliwa sasa kama kanuni ya hukumu. Maneno yanakuwa wazi ili wote waweze kuyasoma. Ukumbusho umeamshwa. Giza ya imani ya mambo ya uchawi na uzushi imesafishwa kwa kila wazo.TSHM 311.1

    Ni vigumu kueleza hofu kuu na kukata tamaa kwa wale waliokanyanga sheria ya Mungu. Kwa kufanya urafiki na ulimwengu, wameweka kando maagizo yake na wakafundisha wengine kuzivunja. Sasa wamehukumiwa kwa sheria ile ambayo wameizarau. Wanaona ya kwamba wanakuwa bila kisingizio. Adui za sheria ya Mungu wanakuwa na wazo mpya juu ya kweli na mapashwa. Kuchelewa sana wanaona ya kwamba Sabato ni muhuri wa Mungu mwenye uhai. Ni kuchelewa sana wanaona msingi wa mchanga ambapo juu yake walijenga. Wamekuwa wakipigana kumpinga Mungu. Waalimu wa dini wameongoza roho kwa jehanum (kupotea milele) walipokuwa wakidai kuwaongoza kwa Paradiso. Ni madaraka makubwa ya namna gani ya watu katika kazi takatifu, matokeo ya kutisha namna gani kwa kutokuamini kwao!TSHM 311.2

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents