Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kujifunza Biblia Mahali Pote

    Usiku waalimu wa vyuo vya vijiji wakasoma kwa sauti kubwa kwa makundi madogo yaliyokusanyika kando ya moto. Kwa juhudi yote roho zingine zikahakikishwa kwa ukweli. “Kuingia kwa maneno yako kunaleta nuru; kunamupa mujinga ufahamu.” Zaburi 119:130.TSHM 89.4

    Wakatoliki walioachia mapadri na watawa kujifunza Maandiko sasa wakawaalika kwa kuonyesha uwongo wa mafundisho mapya. Lakini, wajinga kwa Maandiko, mapadri na watawa wakashindwa kabisa. “Kwa huzuni,” akasema mwandishi mmoja mkatoliki, “Luther alishawishi wafuasi wake kwamba haikufaa kuamini maneno mengine isipokuwa Maandiko matakatifu.” Makundi yakakusanyika kusikia mambo ya kweli yaliyotetewa na watu wa elimu ndogo. Ujinga wa hawa watu wakuu ukafunuliwa kwa kuonyesha uongo wa mabishano yao kwa msaada wa mafundisho rahisi ya Neno la Mungu. Watumikaji, waaskari, wanawake, na hata watoto, wakajua Biblia kuliko mapadri na waalimu wenye elimu.TSHM 89.5

    Vijana wengi wakajitoa kwa kujifunza, kuchunguza Maandiko na kujizoeza wenyewe na kazi bora ya watu wa zamani. Walipokuwa na akili yenye juhudi na mioyo hodari, vijana hawa wakapata haraka maarifa ambayo kwa wakati mrefu hakuna mtu aliweza kushindana nao. Watu wakapata katika mafundisho mapya mambo ambayo yalileta matakwa ya roho zao, na wakageuka kutoka kwa wale waliowalea kwa wakati mrefu na maganda ya bure ya ibada za sanamu na maagizo ya wanadamu.TSHM 90.1

    Wakati mateso yalipoamshwa juu ya waalimu wa ukweli, wakafuata agizo hili la Kristo: “Na wakati wanapo watesa ninyi katika mji huu, kimbilieni kwa mji mwengine.” Matayo 10:23. Wakimbizi wakapata mahali mlango karibu ulifunguka kwao, na waliweza kuhubiri Kristo, wakati mwengine ndani ya kanisa ao katika nyumba ya faragha ao mahali pa wazi. Kweli ikatawanyika kwa uwezo mkubwa usio wa kuzuia.TSHM 90.2

    Ni kwa bure watawala wa kanisa na wa serkali walitumia kifungo, mateso, moto, na upanga. Maelfu ya waaminifu wakatia muhuri kwa imani yao kwa kutumia damu yao, na huku mateso ilitumiwa tu kupanua ukweli. Ushupavu ambao Shetani alijaribu kuunganisha hayo, matokeo yalikuwa wazi kinyume kati ya kazi ya Shetani na kazi ya Mungu.TSHM 90.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents