Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Luther Mbele ya Baraza Tena

    Wakati alipoingizwa tena ndani ya Baraza, alikuwa mwenye ukimya na amani, lakini shujaa mwenye tabia nzuri, kama mshuhuda wa Mungu miongoni mwa wakuu wa dunia. Ofisa wa mfalme akauliza uamuzi wake. Je, alitaka kukana? Luther akatoa jibu lake kwa sauti ya unyenyekevu, bila ugomvi wala hasira. Mwenendo wake ulikuwa wa wasiwasi na wa heshima; lakini akaonyesha tumaini na furaha ambayo ilishangaza makutano.TSHM 71.3

    “Mfalme mwema sana, watawala watukufu, mabwana wa neema,” akasema Luther, “naonekana mbele yenu leo, kufuatana na agizo nililopewa jana. Kama katika ujinga, ningevunja desturi utaratibu wa mahakama, ninaomba munirehemu; kwani sikukomalia katika ma nyumba ya wafalme, bali katika maficho ya nyumba ya watawa.”TSHM 71.4

    Ndipo akasema kwamba katika kazi zake zingine zilizochapwa alieleza habari ya imani na matendo mema; hata maadui zake walizitangaza kuwa za kufaa. Kuzikana ingehukumu kweli ambazo wote walikubali. Aina ya pili ni ya maandiko ya kufunua makosa na matumizi mabaya ya cheo cha Papa. Kuharibu haya ni kuimarisha jeuri ya Roma na kufungua mlango kuwa wazi sana kwa ukosefu wa heshima kwa Mungu. Katika aina ya tatu alishambulia watu waliosimamia maovu yanayokuwako. Kwa ajili ya mambo haya akakiri kwa uhuru kwamba alikuwa mkali zaidi kuliko ilivyofaa. Lakini hata vitabu hivi hataweza kuvikana kwani adui za ukweli wangepata nafasi kwa kulaani watu wa Mungu kwa ukali mwingi zaidi.TSHM 71.5

    Akaendelea, “Nitajitetea mwenyewe kama Kristo alivyofanya: Kama nimesema vibaya, kushuhudia juu ya uovu’ ... Kwa huruma za Mungu, ninakusihi, mfalme asio na upendeleo, na ninyi, watawala bora, na watu wote wa kila aina, kushuhudia kutoka kwa maandiko ya manabii na mitume kwamba nilidanganyika. Mara moja ninapokwisha kusadikishwa kwa jambo hili, nitakana makosa yote, na nitakuwa wa kwanza kushika vitabu vyangu na kuvitupa motoni. ...TSHM 72.1

    “Bila wasiwasi, ninafurahi kuona kwamba injili inakuwa sasa kama kwa nyakati za zamani, ambayo ni chanzo cha taabu na fitina. Hii ni tabia, na mwisho wa neno la Mungu. `Sikuja kuleta salama duniani lakini upanga,’alisema Yesu Kristo. ... Mujihazali kwamba kwa kuzania munazuia ugomvi musitese Neno takatifu la Mungu na kuangusha juu yenu garika la kutisha la hatari kubwa za misiba ya sasa, na maangamizi ya milele.”TSHM 72.2

    Luther alisema kwa Kijeremani; Sasa aliombwa kukariri maneno yaleyale kwa Kilatini. Akatoa tena maneno yake wazi wazi kama mara ya kwanza. Uongozi wa Mungu ulimusimamia katika jambo hili. Watawala wengi walipofushwa sana na makosa na ibada ya sanamu hata mwanzoni hawakuona nguvu ya mawazo ya Luther, lakini kukariri kukawawezesha kuelewa wazi wazi mambo yaliyoonyeshwa.TSHM 72.3

    Wale waliofunga macho yao kwa nuru juu ya ugumu wakakasirishwa na uwezo wa maneno ya Luther. Mnenaji mkuu wa baraza akasema kwa hasira: “Haujajibu swali lililotolewa kwako. ... Unatakiwa kutoa jibu la wazi na halisi. ... Utakana wala hutakana?”TSHM 72.4

    Mtengenezaji akajibu: “Hivi mtukufu mwema na mwenye uwezo sana unaniomba jibu wazi, raisi,aawa sawa, nitakutolea moja, na ni hili: Siwezi kutoa imani yangu kwa Papa ao kwa baraza, kwa sababu ni wazi kama siku ambayo walikosa na mara kwa mara kubishana wenyewe kwa wenyewe. Ila tu nikisadikishwa na ushuhuda wa Maandiko,... Siwezi na sitakana, kwani si salama kwa Mkristo kusema kinyume cha zamiri yake. Ni hapa ninasimamia, siwezi kufanya namna ingine; basi Mungu anisaidie. Amen.”TSHM 72.5

    Ndivyo mtu huyu wa haki alivyosimama. Ukuu wake na usafi wa tabia, amani yake na furaha ya moyo, vilionekana kwa wote alipokuwa akishuhudia ukubwa wa imani hiyo inayoshinda ulimwengu. Kwa jibu lake la kwanza Luther alisema na adabu, kwa hali ya utii kabisa. Watu wa Papa walizania kwamba kuomba wakati ilikuwa tu mwanzo wa kukana. Charles mwenyewe, alipoona hali ya mateso ya mtawa, mavazi yake yasiyokuwa ya zamani, na urahisi wa hotuba yake, akatangaza: “Mtawa huyu hatanifanya kamwe kuwa mpinga imani ya dini.” Lakini ushujaa na nguvu alioshuhudia sasa, uwezo wa akili yake, ukashangaza watu wote. Mfalme aliposhangaa sana, akapaza sauti: “Mtawa huyu anasema bila kuogopa na moyo usiotikisika.”TSHM 72.6

    Wafuasi wa Roma wakashindwa. Wakatafuta kushikilia mamlaka yao, si kwa kukimbilia kwa Maandiko, bali kwa vitisho, inayokuwa kawaida la Roma. Musemaji wa baraza akasema: “Kama hutaki kukana, mfalme na wenye vyeo wa ufalme wataona jambo gani la kufanya juu ya mpinga imani ya diniasiye sikia nashauri.”TSHM 73.1

    Luther akasema kwa utulivu: “Mungu anisaidie, kwani siwezi kukana kitu kamwe.”TSHM 73.2

    Wakamwomba atoke wakati watawala walipokuwa wakishauriana pamoja. Kukataa kutii kwa Luther kungeuza historia ya Kanisa kwa myaka nyingi. Wakakata shauri kwa kumpatia nafasi tena ya kukana. Tena swali likaulizwa. Je, angewezekana mafundisho yake? “Sina jibu lingine la kutoa,” akasema, “kuliko lile nililokwisha kutoa.”TSHM 73.3

    Waongozi wa Papa wakahuzunika kwamba uwezo wao ulizarauliwa na mtawa maskini. Luther alisema kwa wote kwa heshima inayomfaa Mkristo na utulivu, maneno yake hayakuwa na hasira wala masingizio. Akajisahau mwenyewe na kujiona kwamba alikuwa mbele tu ya yeye aliye mkuu wa mwisho sana kuliko wapapa, wafalme, na wafalme (wakuu). Roho ya Mungu ilikuwa pale, kuvuta mioyo ya wakubwa wa ufalme.TSHM 73.4

    Watawala wengi wakakubali wazi wazi haki ya maneno ya Luther. Kundi lingine kwa wakati ule halikuonyesha imani yao, lakini kwa wakati uliokuja wakasaidia bila woga matengenezo.TSHM 73.5

    Mchaguzi Frederic, akasikiliza maneno ya Luther na kuchomwa moyo. Kwa furaha na moyo akashuhudia ushujaa wa mwalimu na kujitawala kwake, na akajitahidi kusimama imara zaidi katika kumtetea. Aliona kwamba hekima ya wapapa, wafalme, na waaskofu inaonekana bure kwa uwezo wa ukweli.TSHM 73.6

    Mjumbe wa Papa alipoona mvuto wa maneno ya Luther, akaamua kutumia njia yote ya uwezo wake ili kumwangamiza Mtengenezaji. Kwa elimu na akili ya ujanja akaonyesha mfalme kijana hatari ya kupoteza urafiki usaada wa Roma kwa ajili ya maneno ya mtawa asiye na maana.TSHM 73.7

    Kesho yake ya jibu wa Luther, Charles akatangaza kwa baraza kusudi lake kwa kudumisha na kulinda dini ya Katoliki. Mashauri ya nguvu yalipashwa kutumiwa juu ya Luther na mambo ya upinzani wa imani ya dini aliyofundisha: “Nitatoa mfalme zangu kafara, hazina zangu , rafiki zangu, mwili wangu, damu yangu, roho yangu na maisha yangu. ... Nitamushitaki na wafuasi wake, kama waasi wapinga imani ya dini, kwa kuwatenga kwa Ushirika takatifu, kwa mkatazo, na kwa namna yo yote iliyofikiriwa kwa kuwaangamiza.” Lakini, mfalme akatangaza, hati ya kupita salama ya Luther inapaswa kuheshimiwa. Anapashwa kuruhusiwa kufika nyumbani mwake salama.TSHM 73.8

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents