Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Hawakutayarishwa Kuingia Mbinguni

    Wale waliochagua Shetani kuwa kiongozi wao hawakutaya-rishwa kuingia machoni pa Mungu. Kiburi, uongo, uasherati, ukali, yamekazwa katika tabia zao. Je, wanaweza kuingia mbinguni kukaa milele pamoja na wale ambao waliwachukia duniani? Kweli haitaweza kuwa ya kupendeza kwa mwongo; upole hautaweza kutuliza kujisifu; usafi hauwezi kukubaliwa kwa mwovu; upendo usiotaka faida hauonekane wa kuvuta kwa mwenye choyo. Ni furaha gani mbingu ingeweza kutoa kwa wale wanaoshughulika sana katika faida za kujipendeza nafsi?TSHM 264.4

    Je, wale ambao mioyo yao imejazwa na uchuki kwa Mungu, kwa kweli na kwa utakatifu, wanaweza kuchanganyika pamoja na makutano ya mbinguni na kujiunga katika nyimbo zao za sifa? Miaka ya rehema ilitolewa kwao, lakini hawakuzoeza moyo wao kupenda usafi. Hawakujifunza kamwe lugha ya mbinguni. Sasa ni kuchelewa.TSHM 264.5

    Maisha ya maasi kumpinga Mungu haikuwastahilisha kwa mbinguni. Usafi wake na amani yangekuwa ni mateso kwao; utukufu wa Mungu ungekuwa moto unaoteketeza. Wangetamani sana kukimbia kutoka mahali pale patakatifu na wangekaribisha vizuri maangamizi, ili waweze kufichwa kutoka usoni pake yeye aliyekufa kwa kuwakomboa. Mwisho wa waovu anaimarishwa kwa uchaguzi wao wenyewe. Kufukuzwa kwao kutoka mbinguni ni kwa kujichagulia wao wenyewe na ni haki na rehema kwa upande wa Mungu. Kama maji ya Garika mioto ya siku kuu inatangaza hukumu ya Mungu kwamba hakuna dawa ya waovu. Mapenzi yao imetumiwa katika maasi. Wakati uzima unapoisha, ni kuchelewa sana kugeuza mawazo yao kutoka kwa uasi hata wa utiifu, kutoka kwa uchuki hata kwa mapendo.TSHM 265.1

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents