Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Tangu Sasa Hata Milele

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Maandiko Rahisi Yanaleta Hakikisho

    Kama Yoane Mbatizaji wahubiri waliweka shoka katika shina la miti na kusihi sana wote kuzaa “matunda yanayofaa kwa toba.” Kwa kuonyesha tofauti kwa uhakikika wa amani na salama vilivyosikiwa kwa mimbara ya watu wengi, ushuhuda rahisi wa Maandiko ukaleta hakikisho ambalo wachache waliweza kabisa kabisa kupinga. Wengi wakamtafuta Bwana kwa toba. Kwa kuacha mapenzi ambayo walishikamana nayo wakati mrefu ya mambo ya kidunia sasa wakatazama mbinguni. Kwa mioyo ya upole na polepole wakajiunga kwa kupaza sauti: “Ogopeni Mungu, na kumutukuza kwa maana saa ya hukumu yake imekuja.”TSHM 177.1

    Wenye zambi wakauliza kwaa machozi: “Ninapashwa kufanya nini ili niokolewe?” Wale waliokosea jirani zao wakajiharakisha kwa kutengeneza kosa. Wote waliopata amani katika Kristo wakatamani kuijulisha kwa wengine. Mioyo ya wazazi ikarudia kwa watoto wao, na mioyo ya watoto kwa wazazi wao. Malaki 4:5, 6. Vizuizi vya kiburi na matengano vikatupiliwa mbali. Maungamo ya kweli yakafanywa. Mahali po pote roho zilikuwa zikiomboleza mbele ya Mungu. Wengi walitumia usiku wote mzima katika maombi kwa ajili ya hakika kwamba zambi zao zilisamehewa, ao kugeuka kwa jamaa zao wala jirani.TSHM 177.2

    Makundi yote, watajiri na maskini, watu wa juu wala wa chini, wakawa na hamu ya kusikia mafundisho ya kuja kwa maraa ya pili. Roho ya Mungu ikatoa uwezo kwa ukweli wake. Kuwako kwa Malaika watakatifu kulisikiwa katika makutano haya, na wengi walikuwa wakiongezeka kila siku kwa waaminifu. Makutano makubwa wakasikiliza kwa utulivu kwa maneno ya heshima. Mbingu na dunia vilionekana kukaribiana. Watu wakarudi nyumbani na sifa kwa midomo yao, na sauti ya furaha ikavuma kwa utulivu wa usiku. Hakuna aliyehuzuria mikutano hiyo angaliweza kamwe kusahau maono ya usikizi mwingi.TSHM 177.3

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents