Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Thibitisha Mambo Yote, Sura ya 147

    Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali.” Mathayo 7:15.Mar 155.1

    kazi ambayo mimi na mume wangu tuliitwa kuishiriki tangu mwanzo wake mnamo mwaka 1843 na 1844 kwa majaliwa ya Mungu, tulimruhusu Mungu abuni na kupanga kwa ajili yetu, naye akatekeleza mipango yake kupitia kwa wanadamu. Mara kwa mara, njia za uongo zilibainishwa kwetu, na njia za kweli na salama zikaelezwa wazi katika shughuli zote ambazo zilihusiana na kazi tuliyopewa kuifanya, kiasi kwamba ninaweza kusema kwa uhakika kabisa kuwa, ninazifahamu vizuri hila za Shetani, na pia njia na kazi za Mungu, Tulipaswa kutumia uwezo wetu wote wa kiakili, tukitumainia hekima ya Mungu kutuongoza katika uchunguzi wetu kwani (ulipaswa kupitia upya nadharia mbalimbali ambazo zililetwa kwetu, tukilinganisha sifa nzuri na kasoro za nadharia hizo kwa nuru ya Neno la Mungu na mambo ambayo Mungu amenifunulia kupitia katika Neno lake na shuhuda, ili kwamba sisi tusidanganywe na wala tusije tukawadanganya wengine. Tulisalimisha nia na njia zetu kwa Mungu, na kuomba kwa bidii ili kupata msaada wake na maombi yetu yalijibiwa. Miaka mingi ya uzoefu mchungu kuhusiana na kazi ya Mungu kumenifanya kufahamu aina zote za vuguvugu za uongo. Mara nyingi nimetumwa kwenda sehemu mbalimbali nikiwa na ujumbe usemao, “Ninayo kazi unayopaswa kuitenda mahali hapo; nami nitakuwa pamoja nawe. Wakali fursa ilipopatikana, Mungu aIinipatia ujumbe kwa ajili ya wale ambao walikuwa wanapata ndoto na njozi za uongo, na katika nguvu za Kristo nilitoa ushuhuda wangu kulingana na agizo la Bwana.Mar 155.2

    Katika kipindi cha miaka arobaini na tano iliyokuwa imepita, nililazimika kukabiliana na watu ambao walikuwa wanadai kuwa na ujumbe wa maonyo kutoka kwa Mungu kwenda kwa watu wengine. Aina hii ya ushupavu wa kidini imekuwa ikijitokeza mara kwa mara langu mwaka 1844. Shetani amefanya kazi kwa njia nyingi ili kuimarisha makosa. Baadhi ya mambo ambayo yalielezwa katika maono hayo yalitimia; lakini mambo mengi - kuhusiana na wakali wa kuja kwa Kristo mara ya pili, mwisho wa rehema, na matukio ambayo yatatokea - yalithibitika kuwa ni uongo mtupu ...Mar 155.3

    “Jiangalieni basi jinsi msikiavyo” (Luka 8:18), ni onyo kutoka kwa Kristo . . . Chunguza kwa karibu zaidi, “jaribuni mambo yote” (1 The. 5:21 ). Huu ndiyo ushauri wa Mungu: je, tutautii?Mar 155.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents