Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kupanda na Kuvuna Katika Maisha, Sura ya 74

  Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafutate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi. 2 Timotheo 2:22.Mar 82.1

  Muda mfupi unaotumika katika kupiga maisha ujanani, rafiki zangu vijana wapendwa, utatoa mazao ambayo yatafanya maisha yako yote yawe machungu; saa moja ya kutowaza yaliyo sahihi, mara unapokubali kuingia katika jaribu, waweza kubadilisha mkondo mzima wa maisha yako kwenda mwelekeo usio sahihi. Unao ujana mmoja tu; hebu ufanye kuwa wenye manufaa. Upitapo katika eneo moja huwezi kurejea na kurekebisha makosa yako...Mar 82.2

  Shetani ...huwa anajigeuza na kuwa mfano wa malaika wa nuru ajapo kwa vijana na majaribu yake yanayohadaa na huwa anafanikiwa kuwashinda, hatua kwa hatua, kutoka katika wajibu wao. Anaelezewa kama mshitaki, mdanganyifu, mwongo, mtesaji na muuaji... Analolitenda Shetani ni kukujaribu na unalolitenda wewe ni kukubali jaribu. Majeshi yote ya Shetani hayakupewa uwezo wa kulazimisha anayejaribiwa kukubali kuasi sheria . Hakuna udhuru wa kutenda dhambi.Mar 82.3

  Jaribu siyo dhambi. Yesu alikuwa matakatifu na safi; bado alijaribiwa katika mambo yote kama sisi, lakini majaribu yalikuja kwa nguvu na msukumo ambao hakuna mwanadamu atategemewa akabiliane nayo. Kutokana na mafanikio yake katika kupambana nayo ametuachia kilelezo kilicho safi, ili tupate kufuata hatua zake. Kama tunajiamini wenyewe au tunajihesabia haki tutaachwa tuanguke katika nguvu ya jaribu; lakini kama tutamwangalia Yesu na kumtegemea Yeye tutakuwa tumeita uwezo uliomshinda adui katika uwanja wa vita kuwa upande wetu, na pamoja na kila jaribu atafanya njia ya kutokea. Shetani anapokuja kwetu kama gharika, tunapaswa kukabiliana na majaribu yake kwa upanga wa Roho, na Yesu atakuwa msaada wetu na atatuinua dhidi yake.Mar 82.4

  Mwenendo mmoja usio sahihi wa tabia, tamaa moja ya dhambi iliyoendekezwa, matokeo yake yatakuwa ni kudhoofishwa kwa nguvu ya injili... Uzito wa majukumu na anasa za dhambi ni kamba azitumiazo Shetani kufunga watu katika mitego yake. Wale walio radhi kufa badala ya kutenda dhambi moja ndiyo pekee watakaokutwa wakiwa waaminifu.Mar 82.5

  Vijana wanaweza kuwa na kanuni zilizo imara sana kiasi kwamba majaribu yaliyo makali zaidi ya Shetani hayataweza kuwavuta toka kwa yule ambaye wamechagua kumtii.Mar 82.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents