Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Njia Kuu Kuelekea Uzimani, Sura ya 102

    Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo. Mathayo 7:13,14.Mar 110.1

    Kristo anatuita tuingie kupitia njia nyembamba, ambapo kila hatua inamaanisha kujikana nafsi. Anatuita tusimame katika jukwaa la ukweli wa milele, kisha tupambane, naam, tupambane kwa dhati, kwa ajili ya imani ambayo ilitolewa kwa watakatifu. . .Mar 110.2

    Tunapozidi kukaribia wakati ambapo wakuu na mamlaka na uovu wa kiroho katika mahali palipoinuka vitakapokuwa pamoja katika vita kamili dhidi ya kweli, wakati nguvu ya Shetani ya udanganyifu itakapokuwa kubwa kiasi kwamba, hata kama ingewezekana, angedanganya hata walio wateule, mtazamo wetu unapaswa kufanywa kuwa wa makini zaidi kutokana na kuangaziwa na uungu, ili tusibaki katika kutojua mbinu za Shetani. . . Kwa kutupatia ushirikiano wa malaika watakatifu, Mungu ametupatia uwezo wa kuifanya kazi yetu iwe ya mafanikio yaliyotukuka. Lakini mara chache sana, kama hili lipo, ambapo mafanikio huwa yanakuja wakati juhudi zinakuwa zimegawanyika. Mvuto wa umoja wa wote walio washiriki wa kanisa unahitajika.Mar 110.3

    Kanisa leo linahitaji watu ambao kama Henoko, wanatembea na Mungu, wakimfunua Kristo kwa ulimwengu. Washiriki wa kanisa wanahitajika kufika katika kiwango cha juu. Wajumbe wa kimbingu wanasubiri kuwasiliana na wale ambao wamezamisha nafsi zao hata zisionekane, wale ambao maisha yao ni utimilifu wa maneno, “lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu: na uhai nilio nao sasa katika mwili ninao katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.” Kanisa linapaswa kuwa na watu wa namna hii ili liweze kutoa nuru yake iliyo na mng’ao wenye miali mikali kwa ulimwengu. Mwonekano wa Jua la Haki kwetu sisi umezuiwa na wingu la ubinafsi. Kristo anasulubiwa upya na wale ambao kupitia kwa mazoea mabaya ya nafsi wanamruhusu Shetani kuwatawala. . .Mar 110.4

    Ni makusudi ya Mungu ya kwamba wote wajaribiwe, ili athibitishe kama ni watii au siyo kwa sheria zinazotawala ufalme wa mbinguni. Hadi mwisho, Mungu anamruhusu Shetani kujifunua mwenyewe kama mwongo, mshitaki, na muuaji. Kwa namna hiyo ushindi wa mwisho wa watu wake unaonekana wazi zaidi, unatukuzwa zaidi na unaondolewa mapungufu na kukamilishwa.Mar 110.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents