Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kazi ya Kimishenari ya Jumapili, Sura ya 170

  Lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho. 2 Timotheo 4:2.Mar 178.1

  Kudharau sheria za Jumapili kutawaimarisha mashabiki wa kidini katika kutesa maana watakuwa wakitafuta namna ya kuzitekeleza. Msiwape nafasi ya kusema kuwa ninyi ni wavunja sheria. Kama wakiachwa ili kudhibiti watu wasiomwogopa Mungu wala watu, udhibiti huo utakosa maana kwao katika muda mfupi sana, na wataona kwamba suala la kuwa wakali katika ushikaji wa Jumapili halina mwelekeo wala halifai. Endeleeni moja kwa moja na kazi yenu ya umishenari, mkiwa na Biblia mikononi mwenu, na adui ataona kuwa amefanya kazi bure. Kwa kuonesha kuwa anatambua hekima ya kutunza amani kwa kuacha kufanya kazi iwezayo kuudhi, mtu hatapokea alama ya mnyama, kwani hata hivyo wakati huo huo atakuwa akifanya kazi yenye umuhimu wa juu zaidi.Mar 178.2

  Tukiiweka Jumapili kuwa ya pekee kwa ajili ya kazi za kimishenari, tutakuwa tumeondoa kiboko toka mikononi mwa mashabiki wasio na msingi ambao watapendezwa kabisa kuwadhalilisha Waadventista wa Sabato. . .Mar 178.3

  Jumapili inaweza kutumika kwa ajili ya kuendeleza sehemu mbalimbali za kazi ambazo zitakamilisha mengi kwa ajili ya Bwana. Katika siku hii mikutano ya hadhara na ile ya nyumbani yaweza kuendeshwa. Kazi ya nyumba kwa nyumba yaweza kufanywa. Waandishi wanaweza kutumia siku hii katika kuandika makala zao. Pale itakapowezekana hebu huduma za kidini zifanyike Jumapili. Ifanyeni mikutano hii iwe ya kuvutia sana. Imbeni nyimbo zilizo makini na za uamsho, na pia mnene kwa nguvu na uhakika kuhusu upendo wa Mwokozi. Semeni kuhusu kiasi na uzoefu wa kweli wa kidini. Kwa jinsi hiyo pia mtajifunza mengi juu ya namna ya kufanya kazi, na mtazifikia roho nyingi...Mar 178.4

  Sheria ya kuadhimisha siku ya kwanza ya juma ni matokeo ya Ukristo ulioasi. Jumapili ni mtoto wa Upapa, ambaye atatukuzwa na ulimwengu wa Kikristo kuliko siku ya Mungu ya pumziko. Kwa namna yoyote watu wa Mungu hawapaswi kuiheshimu. Lakini ninatamani waelewe kuwa hawatakuwa wakifanya mapenzi ya Mungu watakapolazimisha upinzani wakati ambapo Mungu atawahitaji waepuke kufanya hivyo.Mar 178.5

  Mionekano ya ajabu inafunguka mbele yetu; na wakati huu ushuhuda ulio hai unapaswa uonekane katika maisha ya watu wa Mungu, ili ulimwengu upate kuona ya kuwa katika kizazi hiki, wakati uovu unapotawala kila upande, bado wapo watu ambao wataweka pembeni mapenzi yao na watatafuta kutenda mapenzi ya Mungu - watu ambao sheria ya Mungu imeandikwa ndani ya mioyo na maisha yao. Mar 178.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents