Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Zahama Iliyo Mbele, Sura ya 60

    Ole wake siku hii! Kwa maana siku ya BWANA inakaribia, nayo itakuja kama uangamivu utokao kwake aliye Mwenyezi. Yoeli 1:15.Mar 68.1

    Unabii ambao MIMI NIKO aliye mkuu ameutoa katika neno lake, akiunganisha sehemu moja baada nyingine katika mnyororo wa matukio, tokea katika umilele wa wakati uliopita hadi umilele wa wakati ujao, anatuambia pale tuIipo leo katika mtiririko wa vizazi, na kile kinachotegemewa mbeleni. Yote ambayo unabii ulitabiri na kueleza kutimilizwa kwake, hadi wakati huu, yameandikwa katika kurasa za historia, na twaweza kuhakikishiwa ya kwamba yote ambayo hayajatokea yatatimia katika utaratibu wake.Mar 68.2

    Leo dalili za nyakati zinatangaza ya kwamba tunasimama katika kingo za matukio makuu yaliyo mazito. Kila kitu katika dunia yetu sasa kipo katika hali ya msukosuko. Unabii wa Mwokozi wa matukio yanayotegemewa kuwepo kabla ya ujio wake unatimia mbele za macho yetu: “Mtasikia habari za vita na matetesi ya vita...taifa litaondoka kupigana na taifa, na ufalme kupigana na ufalme; kutakuwa na njaa, na matetemeko ya nchi mahali mahali.”Mar 68.3

    Wakati uliopo ni wakati wenye mambo ya kushangaza sana kwa wote walio hai. Watawala na wakuu wa nchi, watu wenye kushikilia nyadhifa za heshima na mamlaka, watu wenye hekima wa viwango vyote, wameweka mtazamo wao katika matukio yanayotuzunguka. Wanatazama mahusiano yaliyopo kati ya mataifa. Wanaona nguvu iliyopo ambayo inatawala kila kitu kwa namna ya kidunia, na wanatambua ya kwamba kitu fulani kikubwa ambacho pia ni hitimisho kinakaribia kutendeka—ya kwamba ulimwengu upo katika ukingo wa zahama ya ajabu.Mar 68.4

    Biblia peke yake, inatoa mtazamo ulio sahihi wa mambo haya. Hapa ndipo yanapofunuliwa matukio makuu ya mwisho ya historia ya ulimwengu...sauti ya ukaribu wake ikisababisha dunia kutetemeka na mioyo ya watu ikizimia kwa hofu.Mar 68.5

    Leo, watu na mataifa wanajaribiwa kwa kipimo kilichopo katika mkono wake Yeye asiyekosea. Kwa kuchagua kwao wenyewe, wote wanaamua hatima yao, na Mungu anaendelea kutawala juu yao kwa ajili ya kukamilisha mapenzi yake.Mar 68.6

    Wakristo wanapaswa kujiandaa kwa ajili ya kile kinachokuja kwa kushtukiza kuuvunja ulimwengu, na hivyo maandalizi haya wanapaswa kuyafanya kwa kuweka bidii katika kujifunza neno la Mungu na kujitahidi kupatanisha maisha yao na kanuni zake.Mar 68.7

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents