Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Mbingu ya Kuitafuta, Sura ya 27

    Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba. Luka 21:36..Mar 35.1

    Siku tunazoishi ni nyeti na muhimu. Roho wa Mungu anaondolewa taratibu lakini kwa uhakika kutoka katika dunia. . .Mar 35.2

    Hali ya mambo duniani inaonesha kwamba nyakati za taabu zinatujia. Magazeti ya kila siku yanaashiria migogoro ya kutisha katika siku zijazo.Mar 35.3

    Unyang’anyi wa wazi linatokea mara kwa mara. Migomo ni jambo la kawaida. Wizi na mauaji yanafanyika na kila mkono. Watu waliopagawa na pepo wanaita watu, wakubwa kwa wadogo. Watu wamezama katika uovu, na kila aina ya uovu inazidi kuongezeka.Mar 35.4

    Kila kitu duniani kiko katika msukosuko. Alama za nyakati zinaashiria kuwa jambo baya litatukia hivi karibuni. Matukio yajayo yanaonesha dalili. Roho wa Mungu anatoweka katika nchi, na janga moja Iinakuja baada ya jingine katika bahari na katika nchi. Kuna dhoruba kali, matetemeko, myoto, mafuriko, mauaji ya kila aina... Watu wanasimama chini ya bendera walioichagua kwa kasi. Wanasubiri na kutazama matendo ya viongozi wao kwa shauku. Wapo wale wanaongoja na kukesha wakijindaa kwa ajili ya kuja kwa Bwana wetu. Kundi lingine wanaangukia chini ya uongozi wa yule mwasi mkuu wa kwanza. Wachache wanaamini kwa moyo kwamba tuna jehanamu ya kuiepuka na mbingu ya kuitafuta.Mar 35.5

    Dhiki inatunyatia taratibu. Jua linaangaza angani, likipita katika njia yake ya kawaida. . . Watu bado wanakula na kunywa, wanapanda na kujenga, kuona na kuolewa. Wachuuzi wananunua na kuuza. Watu wanapigana vikumbo, wakishindania nafasi ya juu zaidi. Wapenda anasa bado wanafurika katika kumbi za maonesho, mashindano ya mbio za farasi, na majumba ya kamari. Msisimko wa hali ya juu kabisa unaendelea, lakini muda wa majaribio unakuisha haraka, na kila shauri linakaribia kuamriwa kwa mara ya mwisho. . .Mar 35.6

    Maneno ya onyo kutoka kwa Bwana katika Mlima wa Mizeituni yanatujia katika kila karne kwa umakini mkubwa: “Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafla.”Mar 35.7

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents