Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Makundi Mawili Makuu ya Wakristo, Sura ya 180

    Nikaona kimoja cha vichwa vyake kana kwamba kimetiwa jeraha la mauti, na pigo lake la mauti likapona. Ufunuo 13:3.Mar 188.1

    Katika suala la kulipa Upapa heshima kubwa, Marekani haikuwa peke yake. Mvuto wa Rumi katika nchi ambazo zilitambua mamlaka yake, bado una nguvu sana.Mar 188.2

    Katika vita vya mwisho Sabato itakuwa ndiyo mada ya muhimu ya pambano katika ulimwengu wote wa Kikristo. Watawala wa kidunia na viongozi wa kidini wataungana ili kushinikiza uadhimishaji wa Jumapili; na kutokana na kushindwa kwa hatua zilizo dhaifu, sheria zinazokandamiza zitatekelezwa. Itasisitizwa kwamba wale wachache wanaopinga taasisi ya kanisa na sheria ya nchi hawapaswi kuvumiliwa. . . Rumi inayotokana na wakati uliopita na Uprotestanti ulioasi uliomo katika wakati huu, zitapambana kwa pamoja katika haraka i ya kukabiIi wale wanaoheshimu kanuni za kimbingu.Mar 188.3

    Ulimwengu unaoitwa wa “Kikristo” utakuwa kama uwanja wa maonesho wa matendo makuu na ya wazi. Watu wenye mamlaka watatekeleza sheria zinazotawala dhamiri, kulingana na kielelezo cha Upapa. Babeli itayafanya mataifa yote kunywa mvinyo ya ghadhabu ya uasherati wake. Kila taifa litahusika.Mar 188.4

    Onyo la malaika yule wa wa tatu [la Ufunuo 14]. . . Linawakilishwa katika unabii kama inatangazwa kwa sauti kuu, na malaika anayeruka kati ya mbingu; na hivyo litavuta usikivu wa ulimwengu.Mar 188.5

    Katika suala litakalokuwa la ushindani ulimwengu wote wa Kikristo utagawanyika katika makundi makuu mawili — wale wazishikao amri za Mungu na imani ya Yesu, na wale wamwabuduo mnyama na sanamu yake na kupokea alama yake. Ingawa kanisa na serikali vitaunganisha nguvu yao ili kuwashurutisha “wote wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa” (Ufu. 13:16), kupokea “alama ya mnyama,” bado watu wa Mungu hawataipokea. Nabii wa Patino anaona “wale wenye kushinda, watokao kwa yule mnyama, na sanamu yake, na kwa hesabu ya jina lake, walikuwa wamesimama kandokando ya hiyo bahari ya kioo, wenye vinubi vya Mungu. Nao wauimba wimbo wa Musa , mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwana-Kondoo.” Ufu. 15:2,3.Mar 188.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents