Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kulia au Kushangilia?, Sura ya 31

    Mavuno yamepita, wakati wa hari umekwisha, wala sisi hatukuokolewa. Yeremia 8:20.Mar 39.1

    Nawasihi washiriki wa makanisa yetu kutopuuzia kutimia kwa ishara za nyakati, ambazo zinaonesha wazi kuwa mwisho u karibu. Hivi karibuni wengi ambao hawakujali wokovu wa roho zao wataomboleza Kwa uchungu wakisema, “Mavuno yamepita, wakati wa hari umekwisha, wala sisi hatukuokolewa.’‘ Tunapaswa kukumbuka kuwa wakati huu ni wa hukumu kwetu, na kwamba kesi zetu zinakuja! Sasa hivi ni wakati wa kuomba na kukesha, kuweka mbali uendekezaji wa nafsi, kiburi chote, na ubinafsi wote. Muda wa thamani ambao unapotezwa na wengi sasa hivi, unapaswa kutumiwa katika tafakari na maombi. Wengi wa wale wanaodai kuwa wanazishika umri za Mungu wanafuata nia zao badala ya kutimiza wajibu. Jinsi walivyo sasa hivi, hawastahili uzima wa milele. Ninataka kuwaambia watu hawa wasiojali, “Mawazo yenu batili, maneno yenu mabaya, matendo yenu ya kibinafsi, yanaandikwa katika kitabu cha mbinguni. Malaika waliokuwa kwenye shamarashamara za kipagani za Belshaza, wamesimama kando yenu mnapomvunjia heshima Mwokozi wenu. Wanageuka kwa huzuni, kwa kuwa mnamsulibisha mara ya pili, na kumfedhehi dhahiri....”Mar 39.2

    Siku ya kutawazwa kwa Kristo, atawatambua kuwa ni watu wake, wale ambao hawatakuwa na doa wala kunyanzi au jambo kama hilo. Na waaminifu wake atawapa taji ya utukufu wa uzima. Wale ambao hawakutaka awatawale watamwona akiwa amezungukwa na jeshi la waliokombolewa, kila mmoja akiwa na ishara isemayo, “Bwana, Aliye Haki Yetu.” Watakiona kichwa ambacho wakati fulani kilikuwa kimevikwa taji ya miiba, kikiwa kimevikwa taji ya utukufu.Mar 39.3

    Katika siku hiyo, waliokombolewa watang’aa katika utukufu wa Baba na Mwana wake. Malaika wa mbinguni wakipiga vinubi vyao vya dhahabu, watamkaribisha Mfalme pamoja na wale ambao ni tuzo ya ushindi wake— wale waliooshwa na kuwa safi katika damu ya Mwana Kondoo. Wimbo wa ushindi utasikika, ukiijaza mbingu. Kristo ameshinda. Ataingia katika nyua za mbinguni akiwa na wale aliowakomboa, ushuhuda kwamba kazi yake ya kuteseka na kujitoa mhanga haikuwa ya bure.Mar 39.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents