Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ari Potofu, Sura ya 118

  Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa. Warumi 10:2.Mar 126.1

  Kuna juhudi zinazoonekana, lakini hazina malengo wala makusudi, ambazo si katika maarifa, ambazo hazina mwelekeo katika utendaji wake na zinasababisha uharibifu. Hizi si juhudi za Kikristo. Juhudi za Kikristo hutawaliwa na kanuni na si za mlipuko. Ni za dhati, za kina na ni thabiti, zikihusisha kila kiungo na kuamsha matumizi ya hisia za uadilifu.Mar 126.2

  Wokovu wa watu na maslahi ya ufalme wa Mungu ni mambo muhimu kabisa. Je, ni jambo gani Iinalohitaji ari kubwa kuliko wokovu wa watu na utukufu wa Mungu? Kuna mambo ya kuangalia hapa ambayo hayawezi kuchukuliwa juu juu tu. Yana uzito mkubwa kama umilele. Yanahusu mustakabali wa mambo ya milele. Watu wanaamua kuingia ama katika neema au dhiki. Ari ya Kikristo itamwongoza mtu kutojisumbua na maneno tu, bali atajisikia na kutenda kwa bidii na kwa ufanisi. Hata hivyo mtu mwenye ari ya Kikristo hatafanya mambo kwa ajili ya kuonekana. Unyenyekevu utaonekana katika kila juhudi na utaonekana katika kila kazi. Ari ya Kikristo itasababisha maombi na unyenyekevu wa dhati pamoja na uaminifu katika majukumu ya nyumbani. Katika familia kutakuwa na upole na upendo, wema na huruma, ambavyo ni matunda ya ari ya Kikristo. . .Mar 126.3

  Inashangaza kwamba watu wanaoiona thamani ya roho ni wachache sana! Watu walio tayari kujitoa mhanga kwa ajili ya kufanya watu wamjue Kristo ni wachache sana! Watu wanasema sana, wengi wanadai kuwa wana upendo kwa ajili ya roho zinazopotea; lakini maneno matupu hayana thamani yo yote. Juhudi za Kikristo za dhati ndizo zinazotakiwa—juhudi ambazo zitadhihirika kwa kufanya jambo fulani. Watu wote wanapaswa kushughulika kwa ajili ya nafsi zao kwa sasa, na wakisha kuwa na Yesu katika mioyo yao, wataweza kumkiri kwa wengine. Haiwezekani kumzuia mtu aliye na Yesu kumkiri kama ilivyo vigumu kuzuia maji ya mto Niagara yasitiririke katika maporomoko yake.Mar 126.4

  Uzima wa milele unapaswa kusababisha shauku kubwa ya kila Mkristo kuwa mfanyakazi pamoja na Kristo na malaika wa mbinguni katika ule mpango mkubwa wa ukombozi! Hakuna kazi inayoweza kufananishwa na hii! Kwa kila roho inayookolewa, hazina ya utukufu humwendea Mungu na utukufu huo utaonekana juu ya yule aliyeokolewa na pia juu ya yule aliyetumika katika wokovu wake.Mar 126.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents