Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kuishi ili Kuokoa Wengine, Sura ya 101

  Mtu yeyote akitaka kumfuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku anifuate. Luka 9:23.Mar 109.1

  Dhambi ambayo imezoeleka kwa kiasi kikubwa kuliko zote, tena ambayo hututenganisha na Mungu huku ikizaa madhara ya kiroho yaliyo makubwa na yanayoambukiza, ni ile ya ubinafsi. Hakuna namna ambayo mtu aweza kumrudia Bwana kama sio kwa kujikana nafsi. Kwa kweli hatuwezi kufanya lolote sisi wenyewe; lakini. Mungu akitutia nguvu, twaweza kuishi tukitenda mema kwa wengine, na kwa njia hii kukataa uovu wa ubinafsi. Hatuhitaji kwenda nchi za ugenini ili kuonesha tamaa yetu ya kutoa vyote kwa Mungu, na pia kuishi maisha yenye faida na yasiyo na ubinafsi. Twapaswa kufanya haya katika mazingira ya nyumbani, kanisani mwetu, kati ya wale tunaoshirikiana nao wakati wote na wale tunaofanya nao biashara. Hapo hapo katika maisha ya kawaida ya kila siku ndipo ambapo nafsi inapaswa kukanwa na kutawaliwa.Mar 109.2

  Paulo alisema, “ninakufa kila siku.” Kinachopelekea kutufanya washindi ni nafsi zetu kufa kila siku katika shughuli zile ndogo za maisha. Tunapaswa kusahau nafsi katika kutamani kutendea wengine mema. Wengi wamepoa katika kupenda wengine. Badala ya kutimiza wajibu wao kwa uaminifu, wanatafuta anasa kwa ajili yao wenyewe.Mar 109.3

  Kwa hali iliyo nzuri kabisa Mungu anawasisitizia wafuasi wake wawajibike katika kubariki wengine kwa mvuto wao na raslimali zao, pia watafute hekima yake ambayo itawawezesha kufanya yote katika uwezo wao kuinua mawazo na mapenzi ya wale wanaokubali mvuto wao. Katika kuwatendea wengine, ridhaa ya kweli itapatikana, na pia amani katika mioyo ambayo itakuwa zawadi inayoridhisha. Hali wakiwa wamechochewa na tamaa ya juu ya kutenda mema kwa wengine, watapata furaha ya kweli katika kutekeleza kwa uaminifu majukumu mengi ya maisha. Hii italeta zawadi ya thamani zaidi ya ile ya kidunia; kwani kila jambo litokanalo na uaminifu, lisilo la kibinafsi tunalowajibika nalo linatambulika mbele za malaika na hili hung’ara katika rekodi ya maisha.Mar 109.4

  Mbinguni, hakuna atakayewaza juu ya nafsi yake, au kutafuta anasa yake mwenyewe; lakini wote, kwa sababu ya upendo ulio wa kweli na wa dhati watakuwa wakitafuta furaha ya wale watakaokuwa nao Mbinguni. Kama ni tamaa yetu twende tukafurahie pamoja na familia ya mbinguni katika nchi mpya, tunapaswa kutawaliwa na kanuni za kimbingu hapa.Mar 109.5

  Kazi iliyo kuu kuliko zote ipaswayo kufanyika hapa duniani ni kumtukuza Mungu kwa kuishi kulingana na tabia ya Kristo.Mar 109.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents