Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kazi Kuu Kuliko Zote Duniani, Sura ya 91

    Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Marko 16:15.Mar 99.1

    Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri injili kwa kila kiumbe,” ndiyo amri ya Kristo kwa wafuasi wake. Siyo kwamba wote wameitwa kuwa wachungaji au wamishenari katika maana halisi ya maneno hayo; lakini wote waweza kuwa wafanya kazi pamoja naye katika kutoa “habari njema” kwa watu wote. Amri hii imetolewa kwa wote, wakubwa kwa wadogo, wasomi kwa wasio wasomi, wazee kwa vijana.Mar 99.2

    Mabegani mwa kila mmoja ajuaye ukweli wa wakati huu upo wajibu wa kufanya ujumbe huu ufahamike kwa wengine. Watumishi wa Kristo wanawajibika kwa kiasi kikubwa kwa ajili ya hali na wokovu wa dunia. Hawa wanapaswa kuwa watendakazi wenza pamoja na Mungu katika kazi ya kuongoa roho na kuzileta kwa Kristo.Mar 99.3

    Mada inayovutia moyo wa mwenye dhambi ni Kristo, yeye pekee aliyesulubiwa. Katika msalaba wa Kalvari. Yesu anafunuliwa kwa ulimwengu akionesha upendo usio kifani. Mwasilishe hivyo kwa makutano yenye njaa, na nuru ya upendo wake itawavuta watu toka gizani hadi nuruni, toka uasi hadi utii na utakatifu wa kweli. Kumtazama Yesu katika msalaba wa Kalvari kunainua dhamiri isimame dhidi ya ubaya wa kutisha wa tabia ya dhambi kuliko nguvu nyingine yoyote.Mar 99.4

    Je, washiriki wetu hawatakaza macho yao kwa Mwokozi aliyesulubiwa na kufufuka, ambaye kwake matumaini yao yote ya uzima wa milele yamewekwa? Huu ndio ujumbe wetu, hoja yetu, fundisho letu, onyo letu kwa wale ambao hawajatubu, ujumbe wa kutia moyo wale walio na huzuni na tumaini kwa ajili ya kila muumini. Kama twaweza kuamsha tamaa ya watu ambayo itawapelekea kukaza macho yao kwa Kristo, twaweza hata kuketi pembeni, na kuwaomba kuendelea kukaza macho yao kwa Mwana kondoo wa Mungu. . . Yeye ambaye macho yake yamekazwa kwa Yesu ataacha yote. Ubinafsi wake utakufa. Ataamini Neno lote la Mungu, ambalo limetukuzwa na kuinuliwa kwa namna ya ajabu ndani ya Kristo.Mar 99.5

    Ni fursa ya pekee apewayo kila Mkristo, siyo kutegemea tu, bali pia kuhimiza ujio wa Bwana wetu Yesu Kristo. Kama wote wanaokiri jina lake wangezaa matunda kwa utukufu wake, mbegu ya injili ingepandwa katika ulimwengu mzima kwa haraka kiasi cha ajabu. Katika muda mfupi mavuno ya mwisho yangeiva, na Kristo angekuja kukusanya nataka.Mar 99.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents