Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kesi Yako Inayokuja!, Sura ya 85

  Mcheni Mungu, na kumtukuza; kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Ufunuo 14:7Mar 93.1

  Mwaka wa 1844, Kuhani wetu Mkuu aliingia patakatifu sana pa hekalu la mbinguni, ili kuanza kazi ya hukumu ya upelelezi.Mar 93.2

  Vitabu vya taarifa vinapofunguliwa hukumuni, maisha ya wale wote ambao walipata kumwamini Yesu yanapitiwa mbele za Mungu. Akianzia na wale ambao waliwahi kuishi duniani, kuhani wetu anawasilisha kwanza kesi za kila kizazi baada ya kizazi, na kisha kumalizia na walio hai. Kila jina linatajwa, na kila kesi inachunguzwa kwa makini. Majina mengine yanakubaliwa, na yapo yanayokataliwa. Wale ambao dhambi zao zimesalia katika vitabu vya taarifa, bila kutubiwa au kusamehewa, majina yao yatafutwa toka katika kitabu cha uzima. . .Mar 93.3

  Sasa tunaishi katika siku kuu ya upatanisho. Katika huduma halisi ya namna hii, wakati kuhani mkuu anaendelea kufanya upatanisho kwa ajili ya Israeli, wote wanapaswa kuteseka rohoni mwao kwa kutubu dhambi na kunyenyekea mbele za Bwana, ili wasikatiliwe mbali toka kwa watu wake. Kwa namna hiyo hiyo, wote ambao majina yao yamo katika kitabu cha uzima, wanapaswa katika wakati huu, katika siku hizi chache zinazosalia za rehema, watese roho zao mbele za Mungu kwa kusikitikia dhambi na kuwa na toba ya kweli. Sharti pawepo na upelelezi wa moyo ulio wa ndani sana na ufanywao kwa uaminifu. . . Kuna vita ya dhati mbele yao wote wapambanao kushinda mienendo miovu inayoonekana kujaribu kuwatawala. Kazi ya maandalizi ni kazi ya mtu binafsi. Hatuokolewi kwa makundi. Usafi na kujitoa kwa mmoja hakutakidhi mahitaji ya sifa hizi kwa mwingine. . . Sharti kila mmoja ajaribiwe, na akutwe bila doa au kunyanzi au tatizo lolote kama hilo.Mar 93.4

  Wote ambao wametubu dhambi kweli kweli, na wanaidai damu ya Kristo kama kafara ya upatanisho, wameandikiwa msamaha mbele ya majina yao katika vitabu vya mbinguni; kwa namna hiyo wamekuwa washirika wa haki ya Kristo, na tabia zao zinaonekana kupatana na sheria ya Mungu, dhambi zao zitafutiliwa mbali, na wao wenyewe wataonekana kustahili uzima wa milele. Bwana anatangaza,... “Mimi, naam mimi ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe: wala sitazikumbuka dhambi zako.” Isa. 43:25.Mar 93.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents