Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Katika Ushirika na Kristo, Sura ya 103

  Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi; akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote. Yohana 15:5.Mar 111.1

  Mwisho umekaribia! Mungu analiita kanisa kuweka tayari yale ambayo yamesalia. Kama watendakazi pamoja na Mungu, mnawezeshwa na Bwana kuingia kwenye ufalme pamoja na wengine mnaowaleta. Ninyi ni mawakala wa Mungu walio hai, mifereji ya nuru kwa ulimwengu, na mnazingirwa na malaika wa mbinguni wakiwa na utume toka kwa Kristo ili kuwatunza, kuwaimarisha, na kuwainua mtendapo kazi ya kuokoa roho. . .Mar 111.2

  Simameni mkiwa mmejitenga kwa kuwa tofauti na ulimwengu, na wala msiwe wa ulimwengu, bali mwakisi miali angavu ya Jua la Haki, mkiwa safi, watakatifu, wasio na mawaa, na kwa imani mkiibeba nuru katika njia zote kuu na vichochoro vya dunia.Mar 111.3

  Hebu makanisa yaamke kabla ya kuchelewa milele. Hebu kila mshiriki awe makini na kazi yake binafsi na kuthibitisha jina la Bwana aliloitiwa. Hebu imani na utauwa wa dhati uchukue nafasi ya uzembe na kutokuamini. Imani inapokuwa imeshikamana na Kristo, kweli italeta amani rohoni, na huduma za kidini hazitadoda na kukosa mvuto. . . Unapodumu katika kuishi Kikristo kama unavyojiita, kila siku utakuwa na uzoefu mpya na mkubwa na wenye dhambi wataongolewa. . .Mar 111.4

  Laiti wote wangeamka na kulishuhudia ulimwengu ya kwamba imani yao ni imani iliyo hai, ya kwamba suala zito la muhimu sana IinaikabiIi dunia, kwamba Yesu anakuja upesi. Hebu watu washuhudie kwamba tunaamini ya kuwa tumo katika kingo za ulimwengu wa milele.Mar 111.5

  Ujenzi wa ufalme wa Mungu hapa duniani unadumazwa na kutokuwa waaminifu kwa wanadamu ambao ni mawakala wa kazi yake. Vivyo hivyo ujenzi huo huwa unaendelezwa kutokana na uaminifu wa mawakala hao. Kazi yawezakuzuiliwa kutokana na kushindwa kwa ushirikiano kati ya watu na uungu. Watu waweza kusali “Ufalme wako uje. Mapenzi yako yatimizwe hapa duniani, kama huko mbinguni”; lakini kama wakishindwa kutenda yale yaliyo ya sala hii katika maisha yao, maombi yao hayatakuwa na faida yoyote. Lakini hata ujapokuwa dhaifu, mkosaji, na mwenye dhambi, Bwana anakupatia fursa ya kuingia katika ubia na Yeye mwenyewe. Anakualika uingie katika maelekezo ya kimbingu. Kwa kuungana na Kristo, waweza kutenda kazi za Mungu. “Pasipo mimi”, Kristo alisema, “ninyi hamwezi kufanya neno lolote”.Mar 111.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents