Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Maisha Mapya, Sura ya 62

    Amin, amin, nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu...Hamna budi kuzaliwa mara ya pili. Yohana 3:5-7.Mar 70.1

    Yeye ajaribuye kufika mbinguni kwa uwezo wa matendo yake binafsi katika kuishika sheria anajaribu kitu kisichowezekana. Hakuna usalama kwa mtu ambaye anayo dini ya matendo, ambayo kawaida ni mfano wa utauwa. Maisha ya Kikristo siyo ukarabati au uboreshwaji wa maisha ya zamani, bali ni badiliko la asili. Hapa kuna kufa kwa nafsi na dhambi, na maisha mapya kabisa. Badiliko hili laweza kuletwa tu na utendaji mahiri wa Roho Mtakatifu. . .Mar 70.2

    Yawezekana mtu asiweze kueleza wakati na mahali halisi, au hata kufafanua hatua zote ndogo ndogo za mazingira yaliyopelekea kukamilika kwa mchakato wa uongofu; lakini hili halimfanyi afikiriwe ya kwamba hajaongoka. Kwa kutumia wakala wa aina yoyote hata asiyeonekana kama ulivyo upepo, Kristo anatenda kazi kwa kudumu katika moyo wa mtu. Kidogo kidogo, yawezekana isiwe kwa namna ambayo mpokeaji anaitambua, fikra huwekwa ambazo hatimaye huivuta roho kwa Kristo... Ghafla, Roho anapokuja akiwa na mwito wa moja kwa moja, roho yenyewe inajitoa kwa furaha kwa Yesu. Wengi wameita tukio kama hili uongofu wa ghafla: lakini ni matokeo ya mvuto wa muda mrefu wa Roho wa Mungu,-- mchakato ulio mrefu na wa uvumilivu.Mar 70.3

    Hata ingawa upepo wenyewe hauonekani, huonesha matokeo ambayo huwa dhahiri na kuhisika. Kwa hiyo, kazi ya Roho wa Mungu katika roho ya mtu itajionesha yenyewe katika kila tendo la mtu ambaye amehisi nguvu yake inayookoa. Wakati Roho wa Mungu anapotawala moyo, anabadilisha maisha. Mawazo ya dhambi hutupiliwa mbali, matendo ya uovu liliachwa; upendo, unyenyekevu, na amani huchukua nafasi ya hasira, wivu na ugomvi. Furaha huchukua nafasi ya huzuni, na mwonekano huakisi nuru ya mbinguni. Hakuna aonaye mkono wa yule ainuaye mzigo husika, au aonaye nuru ikishuka toka hekaluni mbinguni. Baraka huja wakati kwa imani roho inapojitoa yenyewe kwa Mungu. Ndipo ile nguvu ambayo hakuna jicho la kibinadamu liwezalo kuiona huumba sura mpya ya Mungu.Mar 70.4

    Haiwezekani kwa mawazo yenye ukomo kuelewa kazi ya ukombozi. Siri yake inazidi ufahamu wa kibinadamu; hata hivyo yeye atokaye mautini kwenda uzimani anatambua ya kwamba hili ni tendo halisi la kiungu. Tunaweza kujua hapa mwanzo wa ukombozi kupitia kwa uzoefu wetu binafsi. Matokeo yake yanadumu milele.Mar 70.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents