Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ufunguo wa Historia, Sura ya 7

  Ee mlinzi, habari gani za usiku? Mlinzi akasema, Mchana unakuja na usiku pia; mkitaka kuuliza, ulizeni; njoni tena. Isaya 21:11 (sehemu ya mwisho), 12.Mar 15.1

  Kueleweka kwa tumaini la kuja kwa Kristo mara ya pili ni ufunguo unaofungua historia yote inayofuata, kisha hueleza masomo ya siku za usoni.Mar 15.2

  Sauti ya mlinzi wa kweli inahitajika isikike sasa katika nchi yote, “Mchana unakuja, na usiku pia.” Tarumbeta yapaswa itoe sauti inayoeleweka, kwani tupo katika siku kuu ya maandalio ya Bwana.Mar 15.3

  Kweli juu ya unabii zimefungwa pamoja, na tunapoendelea kujifunza, zinatengeneza kama kishada kizuri sana cha ukweli wa matendo ya Kikristo. Ni wazi kuwa mahubiri na mafundisho yote tunayotoa hudhihirisha kwamba tunasubiri, tunatendea kazi, na kuombea ujio wa Mwana wa Mungu. Ujio wake ndilo tumaini letu. Tumaini hili lapaswa kufungwa pamoja na maneno na kazi zetu, pamoja na jumuiya zetu na mahusiano yetu. . .Mar 15.4

  Kuja kwa Mwana wa Adamu mara ya pili kunapaswa kuwa neno kuu linalodumu mbele za macho ya watu. Hili ni fundisho ambalo halipaswi liachwe katika mahubiri yetu. Uhalisi wa Milele unapaswa udumishwe kama wazo kuu ndani yetu, ndipo mivuto ya kidunia itaonekana katika uhalisi wake wa kutokuwa na faida na pia ubatili.Mar 15.5

  Sisi ni wageni na wasafiri ambao tunangojea, tunatumaini, na tunaomba kwa ajili ya tumaini lenye baraka, na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, aliye Bwana na Mwokozi wetu. Kama tukiamini hivyo na kuliishi tumaini hili maishani mwetu, imani na tumaini hili vitaamsha utendaji halisi katika maisha yetu; vitaamsha upendo wa kweli kati yetu; maisha matakatifu kwa ajili ya utukufu wa Mungu; na katika matarajio yetu ya kupatiwa thawabu, tofauti kati yetu na ulimwengu itaonekana dhahiri ...Mar 15.6

  Ukweli kwamba Kristo anakuja hauna budi kuwekwa wazi mbele ya kila mtu.Mar 15.7

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents