Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kutengenezwa Katika Karakana ya Mungu, Sura ya 72

    Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Basi mtukuzeni Mungu katika miili yenu. 1 Wakorintho 6:19, 20.Mar 80.1

    Sisi si mali yetu wenyewe. Tumenunuliwa kwa thamani, hata kufikia kiasi cha mateso na kifo cha Mwana wa Mungu. Kama tungeelewa hili, na kulitambua kikamilifu, tungehisi wajibu mkubwa ulio mabegani mwetu wa kujitunza katika hali nzuri zaidi kiafya, ili tutoe kwa Mungu huduma iliyo kamili. . .Mar 80.2

    Bila ya shaka tunaamini ya kwamba Kristo anakuja upesi.... Hatuna shaka, na wala hatujawa na mashaka kwa miaka mingi, ya kwamba mafundisho tunayoyashika hata sasa ndio ukweli wa leo, na kwamba tumekaribia hukumu. Tunajiandaa kumlaki Yeye ambaye atatokea katika mawingu ya mbinguni akiwa na msafara wa malaika kuwapa kutokufa waaminifu na wenye haki. Wakati anapokuja haji ili kututakasa toka dhambini, au kutuondolea dosari katika tabia zetu, au kutuponya toka katika upungufu uliomo katika mienendo na silika zetu. Ikifanywa naye kwa namna yoyote ile, kazi hii itakuwa imekamilika kabla ya wakati huo.Mar 80.3

    Kristo atakapokuja, wale walio watakatifu watadumu kuwa watakatifu. Wale ambao watukuwa wakidumu katika kutunza miili na roho zao katika utakatifu, katika utakaso na heshima, hapo ndipo watakapopokea mguso wa mwisho wa kutokufa. Bali wale wasio wenye haki, wasiotakaswa, na wachafu watasalia katika hali hiyo milele. Hakuna kazi itakayofanywa kwa ajili yao ili waondolewe mapungufu yao na kuwapa tabia takatifu... Haya yote yanapaswa kufanyika sasa katika saa hizi za rehema. Kazi hii inapaswa kukamilishwa kwa ajili yetu. . .Mar 80.4

    Tumo katika karakana ya Mungu sasa. Wengi wetu ni mawe machafu yasiyo na ulinganifu yatokayo katika machimbo. Lakini tunapoendelea kushikilia ukweli wa Mungu, mvuto wake unatuathiri. Unatuinua na kutuondolea kila namna ya upungufu na dhambi. Kwa namna hiyo tunaandaliwa kumuona Mfalme katika uzuri wake na hatimaye kuungana na malaika walio safi wa mbinguni katika ufalme wa utukufu. Kazi hiyo inapaswa ikamilike kwa ajili yetu hapa, ni hapa ambapo miili yetu na roho zetu vinapaswa kufanywa tayari kwa ajili ya hali ya kutokufa.Mar 80.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents