Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Vijana na Tatizo la Madawa ya Kulevya, Sura ya 131

    “Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na katika maono ya macho yako; lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni.” Mhubiri 11:9.Mar 139.1

    Shetani alikuwa ni mwasi wa kwanza ulimwenguni, na tangu alipofukuzwa kutoka mbinguni, amekuwa akitafuta kumfanya kila mwanadamu awe mwasi dhidi ya Mungu sawa naye. Aliandaa mpango wake wa kumwangamiza mwanadamu, na kwa njia ya kuendekeza tamaa ya chakula isivyo halali, Shetani alimwongoza mwanadamu kuasi amri za Mungu. Aliwajaribu Adamu na Hawa kula matunda ya mti waliokatazwa, na hivyo akafanikisha anguko lao na kufukuzwa kwao kutoka Edeni. Ni wangapi wanasema, “Kama mimi ningekuwa ndiye Adamu, nisingeweza kuasi kwa jaribu dogo kama lile.” Lakini ninyi mnaojivuna hivyo mnayo fursa kubwa ya kuonesha uthabiti wa kusudi lenu na uaminifu wenu katika kanuni hata ninapokuwa mkijaribiwa . . . Je, Mungu haoni dhambi yo yote katika maisha yako?. . .Mar 139.2

    Kila upande Shetani anatafuta kuwanasa vijana katika njia ya uangamivu; na kama akifaulu mara moja kuwaingiza katika njia hiyo, anawaharakisha katika hatua nyingine kwenye njia hiyo ya anguko, akiwaongoza toka uovu mmoja hadi mwingine, hadi wahanga hawa wanapokuwa wamepoteza kabisa wororo wa dhamiri zao na kutokuwa tena na hofu ya Mungu machoni pao. Wanakuwa watu wasiojizuia. Wanakuwa na mazoea sugu ya kutumia pombe na mvinyo, tumbaku na kasumba, nao wanakwenda toka hatua moja ya udhalili hadi hatua nyingine. Wao ni watumwa wa tamaa ya chakula. Mashauri ambayo zamani waliyaheshimu sasa wanayadharau. Ni wagomvi, wenye kiburi, na wanajivunia uhuru wakati wao ni watumishi wa uharibifu. Kwa kudai kuwa wako huru wanamaanisha kuwa wao ni watumwa wa ubinafsi, ulafi na uasherati.Mar 139.3

    Shetani amedhamiria kuwafanya wanadamu wote wawe chini yake, lakini Kristo amelipa gharama isiyo na kifani ili mwanadamu aokolewe kutoka kwa adui, na tabia ya Mungu iweze kurejeshwa ndani ya jamii ya binadamu. . . Kupitia kwa Kristo, wanadamu walioanguka dhambini wanaweza kupata njia ya kumkaribia Baba, na kupewa neema ambayo itawawezesha kushinda kwa njia ya ustahili wa Mwokozi aliyesulibiwa na akafufuka.Mar 139.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents