Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Uwe Macho Dhidi ya Hila za Shetani, Sura ya 82

  Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. Nanyi mpingeni huyu, mkiwa thabiti katika imani. 1 Petro 5:8,9.Mar 90.1

  Hebu kila roho iwe macho. Adui yuko katika njia yako. Uwe hodari, na kuwa mwangalifu ili mtego uliofichika na kuwekwa kwa ustadi usije ukakunasa bila wewe kujua. Hebu wale walio wazembe na wasiojali wawe macho siku ile ya Bwana isije wajia kama mwivi usiku. Wengi watatanga mbali na njia ya unyenyekevu, na, huku wakitupilia mbali nira ya Kristo, watatembea katika njia ngeni. Huku wakiwa wamepofushwa na kuchanganyikiwa, wataiacha njia nyembamba iongozayo kwa jiji la Mungu. . .Mar 90.2

  Yeye ashindaye sharti akeshe; kwani kwa kutumia mitego ya kidunia, makosa, na ushirikina, Shetani anajaribu kupata wafuasi wa Kristo awavute kwake. Haitoshi ya kwamba tunakwepa hatari zinazojionesha ikiwemo mienendo ya hatari. Tunapaswa kuwa karibu zaidi na Kristo, tukitembea katika njia ya kujikana nafsi na kujitoa. Tumo katika nchi ya adui. Yeye aliyetupwa toka mbinguni alishuka na nguvu nyingi. Kwa kutumia kila aina ya mbinu na hila anatafuta namna ya kuteka roho. Tusipodumu kuwa macho tutanaswa kirahisi kama nyara zake kutokana na udanganyifu wake mwingi.Mar 90.3

  Wote wanaouamni ukweli wa wakati huu wanapaswa kutambua ya kwamba kila kitu sasa kimevishwa umakini. Wanapaswa kutenda mambo kulingana na viwango vya siku ya Mungu. Hukumu ya Mungu imekaribia kushuka duniani, na tunapaswa kuwa tayari kwa ajili ya siku ile iliyo kuu.Mar 90.4

  Muda tulio nao ni wa thamani kubwa. Tunazo siku chache za rehema ambazo kwazo tunapaswa kufanya maandalizi kwa ajili ya maisha yajayo, maisha yasiyokoma. Hatuna muda wa kutumia katika miondoko isiyo na utaratibu. Tunapaswa kuogopa kuangalia neno la Mungu kwa juu juu tu.Mar 90.5

  Kama shauku yako yote iko katika ukweli na kazi ya maandalio kwa ajili ya wakati huu, utatakaswa na hiyo kweli na litapokea hali ifaayo kwa ajili ya kutokufa. . .Kazi nzito ya maandalizi sharti iendelee kwa wote wanaoukiri ukweli, hadi tutakaposimama mbele ya kiti cha enzi cha Mungu bila kasoro, bila waa, bila kunyanzi, au chochote cha namna hiyo. Mungu atakutakasa kama utajikabidhi kwa ajili ya mchakato wa utakasaji.Mar 90.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents