Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kupanda Ngazi ya Petro, Sura ya 76

    Naam, na kwa sababu iyo hiyo mkijitahidi sana kwa upande wenu, katika imani yenu tieni na wema, na katika wema wenu maarifa, na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu saburi, na katika saburi yenu utauwa na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo. 2 Petro 1:5-7.Mar 84.1

    Elekeza vijana kwa ngazi ya Petro yenye mizunguko minane, na kisha uweke miguu yao katika ule wa chini zaidi, na wala siyo ule wa juu zaidi, na kisha kwa kuwasihi kwa dhati watie moyo wakwee hadi mwisho juu.Mar 84.2

    Kristo.. ni ngazi. Kitako cha ngazi hii kimesimikwa kikiwa imara duniani katika ubinadamu wake; mzunguko wa juu ulio kilele unafika katika kiti cha enzi cha Mungu katika uungu wake. Ubinadamu wa Kristo unakumbatia ubinadamu ulioanguka, hali uungu wake ukikamata kiti cha enzi cha Mungu. Tunaokolewa kwa kukwea katika mzunguko mmoja baada ya mwingine, tukimwangalia Kristo, tukimng’ang’ania Kristo, huku tukikwea hatua moja baada ya nyingine hadi kufikia kimo cha Kristo, ili kwamba yeye afanywe kwetu kuwa hekima na haki na utakaso na ukombozi. Imani, wema, maarifa, kiasi, saburi, utauwa, upendano wa ndugu na upendo ni mizunguko katika ngazi hii. Mienendo hii yote inapaswa ionekane katika tabia ya Kikristo; “maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe. Maana hivi mtaruzukiwa kwa ukarimu kuingia katika ufalme wa milele wa Bwana wetu, Mwokozi wetu Yesu Kristo.”Mar 84.3

    Hupaswi kufikiri ya kwamba sharti usubiri hadi umekuwa mkamilifu katika mwenendo mmoja kabla ya kujenga mwingine. La; hii ni mienendo ambayo inapaswa ikue pamoja...; kila siku unayoishi, waweza kukamilisha sifa zenye baraka zilizofunuliwa kikamilifu katika tabia ya Kristo....Mar 84.4

    Usitishwe na kiasi cha majukumu upaswayo kuyakamilisha wakati wa maisha yako, kwani hutegemewi kuyatekeleza yote mara moja. Hebu uwezo wote ulio nao uwekwe katika kazi ya siku moja, ukiendeleza kila nafasi ya thamani uliyonayo, tambua na kushukuru kwa ajili ya msaada anaokupa Mungu, na ukwee katika ngazi ya maendeleo moja baada ya nyingine. Kumbuka kuishi vema katika siku uliyonayo maishani mwako, kumbuka ya kuwa Mungu amekupatia siku moja katika kila wakati, na taarifa za kimbingu zitaonesha jinsi ulivyothamini fursa na nafasi ulizozipata katika kila siku. Hebu endelea katika kila siku akupayo Mungu kwa namna hiyo, ili hapo mwisho umsikie Bwana akisema, “vema, mtumwa mwema na mwaminifu.”Mar 84.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents