Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Jitahidini Kuongoa Japo Roho Moja,Sura ya 21

    Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aende akamtafute yule aliyepotea hata amwone? Luka 15:4.Mar 29.1

    Tunapaswa kutumia raslimali zetu mpaka mwisho kwa ajili ya kuongoa roho moja. Roho moja ikiongolewa kwa ajili ya Kristo itaangaza nuru ya mbinguni mahali iIipo, na kupenyeza katika giza na kuokoa roho zingine.Mar 29.2

    Kama Kristo aliwaacha wale tisini na tisa, ili amtafute na kumwokoa yule kondoo aliyepotea, je, sisi tunaweza tukawa na udhuru tusipofanya hivyo? Je, kupuuza kufanya kazi kama Kristo alivyofanya na kupuuza kujitoa mhanga kama Yeye alivyojitoa, si usaliti wa dhamana takatifu na kufuru kwa Mungu?Mar 29.3

    Pigeni kelele katika upana na urefu wote wa dunia. Waambieni watu kuwa siku ya Bwana i karibu na inakuja upesi. Asibaki hata mtu mmoja ambaye hajaonywa. Inawezekana tumekuwa mahali penye roho duni zilizo katika makosa. Inawezekana tumekuwa miongoni mwa watu wasiostarabika. Kulingana na ukweli tulioupata kuliko watu wengine, tunawiwa kuutoa ukweli huo kwao.Mar 29.4

    Hatuna muda wa kupoteza. Mwisho umekaribia. Njia za kwenda sehemu mbali mbali kupeleka ujumbe sitazibwa hivi karibuni kwa hatari kila upande, kulia na kushoto. Mambo mbali mbali yatawekwa ili kuwakwamisha wajumbe wa Bwana, ili wasiweze kufanya yale yanayowezekana kwao kuyafanya kwa sasa. Tunapaswa kuingalia kazi yetu kwa dhati na kusongambele kwa haraka kadiri iwezekanavyo katika vita vikali. Kutokana na nuru ambayo nimepewa na Mungu, nguvu za giza zinafanya kazi kwa nguvu kubwa kutoka chini na Shetani anasonga mbele kwa kunyatia ili awatwae, wale ambao wamelala, kama mbwa mwitu aehukuavyo windo lake. Tuna maonyo ambayo tunaweza kuyatoa sasa, kazi ambayo tunaweza kuifanya sasa; lakini hivi karibuni itakuwa vigumu kuliko tunavyoweza kufikiria. Mungu atusaidie kubakia katika nuru, kufanya kazi huku macho yetu yakiwa yameelekezwa kwa Yesu ambaye ni kiongozi wetu, na kusonga mbele kwa saburi huku tukipata ushindi.Mar 29.5

    Katika maisha yetu ya hapa duniani, japo yameharibiwa na dhambi, furaha kubwa na elimu ya juu kabisa ipo katika huduma. Na katika hali ya baadaye, furaha yetu kubwa kabisa na elimu yetu ya juu kabisa itapatikana katika huduma.Mar 29.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents