Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kuwa na Nguvu au Kudumaa Kiroho?, Sura ya 45

  Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu. 2 Wakorintho 7:1.Mar 53.1

  Mungu anakemea na kusahihisha wale wanaodai kushika Sheria yake. Yeye anawaonesha dhambi zao na kuweka wazi uovu wao kwa sababu anatamani kuwatenganisha na dhambi yote na uovu ili utakatifu wao ukamilike katika kumcha na wawe tayari kufa katika Bwana au kubadilishwa na kwenda mbinguni...Mar 53.2

  Mungu hatakubali chochote kilicho pungufu ya usafi na utakatifu; doa moja, kunyanzi moja, upungufu mmoja katika tabia, utawazuia daima wasiingie mbinguni, palipo na utukufu na hazina zote.Mar 53.3

  Wengi wanaodai kuwa Wakristo hawajui kwamba nia, ukereketwa na ustahimilivu ambao wanauonesha katika kukusanya vitu dhaifu vya maisha haya vinavyoharibika, wangeuweka katika kutafuta mambo ya Mungu. Wengi wanaojiita Wakristo wameridhika kuwa mbilikimo kiroho. Hawana azma ya kulipa umuhimu suala la kuutafuta kwanza ufalme wa Mungu na haki yake; matokeo yake utauwa unabaki kuwa fumbo IiIilofichika kwao, hawawezi kuuelewa. Hawamjui Kristo katika uhalisia wa maisha.Mar 53.4

  Mahitaji yote yameshatolewa kwa ajili ya wote ambao kwa uaminifu na kwa kufikiria vema, wameipa umuhimu unaostahili kazi ya kufanywa watakatifu katika kumcha Mungu. Uwezo, neema na utukufu vimetolewa kupitia kwa Kristo, ili viletwe na malaika watakatifu kwa wale warithi wa wokovu. Hakuna aliye mzembe, mchafu, au mwovu, asiyeweza kupata nguvu, utakaso na haki, katika Yesu aliyekufa kwa ajili yao, ikiwa atakoma kuelekea katika njia zake mbovu, na kumgeukia Mungu aliye hai kwa moyo wote. Mungu anasubiri kuwavua mavazi yao, yaliyotiwa madoa na kuchafuliwa na dhambi, na kisha kuwavisha vazi jeupe, la hakika linalong’aa; Anawatia moyo waishi na wasife. Kwake yeye watachanua. Matawi yao hayatanyauka wala kukosa matunda. Kama wakidumu kwake, watapata lishe na virutubisho toka kwake, watajazwa na Roho wake, watatembea kama alivyotembea, watashinda kama alivyoshinda, na watainuliwa na kuwekwa kuumeni kwake.Mar 53.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents