Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Hakuna Nafasi ya Kufanya Kazi ya Shetani, Sura ya 55

  Basi, kwa kuwa vitu hivi vyote vitafumuliwa hivyo, imewapasa ninyi kuwa watu wa tabia gani katika mwenendo mtakatifu na utauwa, mkitazamia hata ije siku ile ya Mungu. 2 Petro 3:11, 12Mar 63.1

  Ni muhimu kwamba wote wajue mazingira ya roho zao, kama wako katika ubia na adui wa haki, na hivyo wakitenda kazi yake kwa kujua, ama kama wamefungamana na Kristo, wakiitenda kazi yake. . .Mar 63.2

  Shetani angefurahia kumweka kila mtu upande wake katika kazi ya kudhoofisha imani ya ndugu na ndugu, na hivyo akipanda mbegu ya kutoelewana kati ya wale wanaodai kuuamini ukweli. Shetani aweza kukamilisha kusudi lake kwa mafanikio makubwa kupitia kwa wale wanaojiita marafiki wa Kristo ambao hawatembei na kutenda kazi kulingana na miongozo ya Kristo. . .Mar 63.3

  Hii ni siku ya maandalizi ya Bwana. Muda haupo sasa kwa ajili ya kuzungumzia kutokuamini au. . . kufanya kazi ya mwovu. Hebu kila mmoja awe makini dhidi ya kudhoofisha imani ya wengine kwa kupanda mbegu za husuda, wivu na utengano; kwani Mungu anasikia maneno, na anahukumu, siyo kwa utetezi wa Ndiyo na Hapana, bali kwa matunda ya kazi ya yule anayehukumiwa. . .Mar 63.4

  Bado pepo nne zinazuiliwa hadi hapo watumishi wa Mungu watakapokuwa wametiwa muhuri katika vipaji vya nyuso zao. Kisha mamlaka za dunia zitajikusanya kwa pambano kuu la mwisho. Tunapaswa kuwa waangalifu sana katika kutumia kipindi kifupi cha rehema kiIichosalia! Twapaswa kujitathmini wenyewe kwa dhati kiasi kikubwa sana!. . .Mar 63.5

  Nidhamu ya roho, usafi wa moyo na mawazo ndivyo vinavyohitajika. Hivi vina thamani kuliko talanta nzuri, busara au ufahamu. Akili ya kawaida ambayo imefunzwa kutii “asemavyo Bwana,” inafaa sana kwa ajili ya kazi ya Mungu kuliko wale walio na uwezo, lakini hawautumii ipasavyo. . . Watu wanajivunia ujuzi wao wa mambo ya kidunia; lakini kama hawana ujuzi wa Mungu wa kweli, wa Kristo, Njia, Kweli na Uzima, ni wajinga wa kutisha na ujuzi wao utaangamia pamoja nao. Ujuzi wa kidunia una nguvu; bali ujuzi wa Neno, ambalo lina mvuto unaobadilisha mawazo ya kibinadamu, hauharibiki.Mar 63.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents