Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Uamsho Bandia, Sura ya 160

    “Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa ufunuo wa kuwepo kwake; yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano Wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara, na ajabu za uongo.” 2 Wathesalonike 2:8, 9.Mar 168.1

    Katika waraka wake wa pili kwa Wathesalonike Paulo anasonda kidole kwa utendaji maalumu wa Shetani katika umizimu kama tukio litukialo kabla ya kurudi kwa Kristo. Tukiongea kuhusu kurudi kwa Kristo, anatangaza kuwa “yule ambaye kuja kwake ni kwa mfano wa kutenda kwake Shetani, kwa uwezo wote, na ishara na ajabu za uongo.” 2 The. 2:9.Mar 168.2

    Kabla ya kumwagwa kwa ghadhabu ya mwisho ya Mungu juu ya dunia kutakuwepo miongoni mwa watu wa Mungu uamsho wa uchaji Mungu halisi ambao haujawahi kushuhudiwa tangu zama za mitume. Roho na uweza wa Mungu utabubujika juu ya watoto wake. Wakati huo wengi watajitenga kutoka makanisa ambamo upendo wa dunia hii umetwaa mahali pa upendo wa Mungu na Neno lake. Wengi, wachungaji kwa waumini, kwa furaha watazipokea kweli kuu ambazo Mungu ameruhusu zitangazwe wakati huu kuandaa watu kwa kurudi kwa Bwana. Adui wa roho anatamani kukwamisha kazi hii; na kabla wakati haujawasili kwa vuguvugu hilo kutokea, atajaribu kulikwamisha kwa kuanzisha uamsho bandia. Yale makanisa anayoweza kuyaweka chini ya udanganyifu wake atafanya ionekane kuwa baraka maalumu ya Mungu imebubujika; kutakuwepo vuguvugu la namna yake litakalotambulika kama uamsho wa kidini. Wengi watashangilia kuwa Mungu anatenda miujiza kwa ajili yao, wakati utendaji huo linaongozwa na yule roho mwngine. Kwa joho la kidini la kujifanya , Shetani atatafuta kuendeleza mvuto wake ndani ya ulimwengu wa Kikristo.Mar 168.3

    Vijana wa kiume na wa kike watainuka, wakijiona wamebarikiwa mno, kuitwa kutenda mambo makubwa. Kutakuwepo uongofu mkuu, kwa jinsi pekee, ila haitakuwa na ukubali wa kimbingu. Zinaa na ubadhirifu vitaingia na wengi watayumba kiimani.Mar 168.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents