Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Pumzi ya Roho, Sura ya 77

  Ombeni bila kukoma. 1 Wathesalonike 5:17Mar 85.1

  Maombi ni pumzi ya roho, mfereji wa baraka zote. Roho inayotubu inapotoa sala yake, Mungu anaona mapambano yake, anaona migogoro yake na kutambua udhati wake. Yeye anaweka kidole chake juu ya mshipa wake wa damu, na anahesabu kila pigo la moyo. Hakuna hisia inayoifurahisha roho hii, wala jambo linaloiudhi, wala huzuni inayoifunika, au dhambi inayoichafua, wala wazo au kusudi linaloiamsha, ambalo Yeye halijui. Roho hii ilinunuliwa kwa thamani isiyopimika, na inapendwa kwa upendo usioelezeka.Mar 85.2

  Ombi linalomwelekea Tabibu Mkuu kwa ajili ya kuponywa kwa roho huwa Iinaleta baraka ya Mungu. Sala zinatuunganisha sisi na Mungu na wenzetu. Sala zinamleta Yesu upande wetu, na zinatupatia nguvu mpya na neema mpya kwa roho iliyochoka na kufadhaishwa...Mar 85.3

  Kristo Mwokozi wetu alijaribiwa katika mambo yote kama sisi, lakini Yeye hakutenda dhambi. Aliichukua asili ya ubinadamu, akiwa katika umbo la mtu, na mahitaji yake yalikuwa mahitaji ya mwanadamu. Alikuwa na matakwa ya kimwili na hivyo kuhitaji kukidhiwa, na pia uchovu wa kimwili uliohitaji kupozwa. Ilikuwa tu kwa njia ya maombi kwa Baba yake ndivyo alivyoweza kujizatiti kwa ajili ya wajibu wake na majaribu. Siku kwa siku alikwenda katika mizunguko ya wajibu wake, akitafuta kuokoa roho.... Yeye pia alitumia usiku mzima katika sala kwa niaba ya wale waliojaribiwa...Mar 85.4

  Nyakati za usiku ambazo Mwokozi alizitumia mlimani au jangwani zilikuwa muhimu katika kumwandaa Yeye kwa ajili ya majaribu ambayo ilikuwa lazima akutane nayo katika siku zilizokuwa mbele yake. Alihisi hitaji la kufanywa upya na kuimarishwa kwa roho na mwili, ili akutane na majaribu ya Shetani; na wale wanaojitahidi kuishi maisha yake watahisi hitaji kama hili.Mar 85.5

  Anatuambia sisi, “mtu yeyote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake, anifuate.” Kristo mwenyewe ndiye awezaye kutufanya tuweze kuitikia anaposema, “Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo.” Hii ikimaanisha kuwa kila siku sharti nafsi ikanwe. Kristo aweza kutupatia maamuzi yenye adili, nia ya kuwa tayari kuteseka, na kupambana katika vita vya Bwana tukiwa na nguvu isiyoehoka. Wale walio dhaifu zaidi, wakisaidiwa na neema ya Mungu, wanaweza kuwa na nguvu za kufanywa kuwa zaidi ya washindi.Mar 85.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents