Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kuharakisha Ujio Wake, Sura ya 11

  Kwa maana Bwana atalitekeleza neno lake juu ya nchi, akilimaliza na kulikata. Warumi 9:28.Mar 19.1

  Katika unabii wa kuharibiwa kwa Yerusalemu, Kristo alisema, “Na kwa sababu ya kuongezeka maasi, upendo wa wengi utapoa. Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye atakayeokoka. Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.” Unabii huu litatimia tena. Wingi wa uovu katika siku hizo linafanana na ule wa kizazi hiki. Itakuwa hivyo pia kwa unabii unaohusu kuhubiriwa kwa injili. Kabla ya kuanguka kwa Yerusalemu, Paulo, akiandika kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, alisema kuwa injili ilikuwa imehubiriwa kwa “viumbe vyote vilivyo chini ya mbingu.” Kol. 1:23. Kwa hiyo sasa, kabla ya kuja kwa Mwana wa Adamu, injili ya milele itahubiriwa kwa “kila taifa, na kabila, na lugha, na jamaa.” Ufu. 14: 6, 14. Mungu “ameweka siku atakayowahukumu walimwengu.” Mdo.7:31. Kristo anatuambia siku hiyo itatokea Iini. Hasemi kwamba ulimwengu wote utaongolewa, ila “habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja.” Tunao uwezo wa kuharakisha kurudi kwa Bwana, kwa kuihubiri injili kwa ulimwengu. Hatupaswi kutazamia tu, bali kuuharakisha ujio wa siku ya Mungu. 2 Pet. 3:12. Kama kanisa la Mungu lingefanya kazi liliyotumwa kama Mungu alivyoagiza, ulimwengu wote ungekuwa umekwisha kuonywa, na Bwana Yesu angekuwa amekwisha kuja katika dunia yetu kwa uwezo na utukufu mkuu.Mar 19.2

  Kinachotufanya tuendelee kuwa katika dunia hii ya dhambi na huzuni kwa miaka mingi ni kutokuamini, kuipenda dunia, kutokujitakasa, na mashindano miongoni mwa wale wanaodai kuwa watu wa Bwana. . .Mar 19.3

  Tunaweza tukaendelea kubaki katika dunia hii kwa miaka mingi zaidi kwa sababu ya ukaidi, kama ilivyokuwa kwa wana wa Israeli; lakini kwa ajili ya Kristo, watu wake hawapaswi kuongeza dhambi juu ya dhambi kwa kumtuhumu Mungu juu ya athari za utendaji wao wenyewe usiofaa.Mar 19.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents