Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Taabu Pande Zote, Sura ya 29

    Mtafuteni Bwana, Enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi mliozitenda hukumu zake; itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya Bwana. Sefania 2:3.Mar 37.1

    Hakuna jambo la kusikitisha kama kuwaona wale walionunuliwa kwa damu ya ... wakigeuka na kubeza ujumbe ambao umeletwa kWAO kwa neema katika Injili, wakikataa Uungu wa Kristo, na kuamini hoja zao wenyewe zisizo na msingi. Watakapojaribiwa kwa mateso, dhana zote potofu walizozishika zitayeyuka kama barafu katika jua.Mar 37.2

    Inasikitisha sana kusimama kando ya jeneza la mtu ambaye alikataa wito wa rehema za Mungu! Inasikitisha sana kusema: Mtu huyu amepotea! Mtu huyu angeweza kufikia kiwango cha juu kabisa, na kupata uzima wa milele, lakini alisalimisha maisha yake kwa Shetani, akanaswa katika falsafa batili za wanadamu, na akawa anachezewa na yule mwovu! Tumaini la Mkristo ni nanga ya roho, yenye uhakika na ya kudumu ambayo huingia hadi kwenye hema ya ndani, ambapo Kristo, mtangulizi wetu aliingia kwa ajili yetu. Tuna kazi ya kufanya sisi wenyewe binafsi katika kujiandaa kwa ajili ya matukio makuu yaliyo mbele yetu.Mar 37.3

    Vijana wanapaswa kumtafuta Mungu kwa bidii. Tufani inakuja, na tunapaswa kuwa tayari kukabiliana nayo kwa kuwa na toba mbele za Mungu na kuwa na imani kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Bwana atainuka na kuitikisa nchi kwa nguvu. Tutaona taabu pande zote. Maelfu ya meli zitatupwa katika vilindi vya bahari. Majeshi ya majini yatazama, na maisha ya watu yataangamia kwa mamilioni. Myoto itazuka bila kutarajiwa, na juhudi za wanadamu hazitaweza kuizima. Majumba ya kifalme duniani yatateketea kwa moto. Majanga katika reIi yataongezeka; machafuko, migongano, na vifo vya ghafla vitatokea katika njia kuu za usafiri. Mwisho umekaribia, muda wa kujaribiwa unafikia ukingoni. Hebu tumtafute Mungu maadam anapatikana, tumwite maadam yu karibu! Nabii Sefania anasema: “Mtafuteni Bwana, Enyi nyote mlio wanyenyekevu wa dunia, ninyi mliozitendda hukumu zake; itafuteni haki, utafuteni unyenyekevu; huenda mtafichwa katika siku ya hasira ya BwanaMar 37.4

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents