Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Maandalizi ya Shetani kwa Ajili ya Pambano la Mwisho, Sura ya 154

    “Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake Aliye juu; naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati.” Danieli 7:25.Mar 162.1

    Mnamo zama za Ukristo, adui mkuu wa furaha ya mwanadamu ameifanya Sabato ya Amri ya nne iwe mlengwa wa mashambulio. Shetani asema, “Nitatenda kushindana na Mungu. Nitawawezesha wafuasi wangu kutupilia mbali kumbukumbu ya Mungu, Sabato ya siku ya saba. Hivyo nitauonyesha ulimwengu kuwa siku iliyotakaswa na kubarikiwa na Mungu imebadilishwa. Siku hiyo isidumishwe akilini mwa watu. Nitafuta kumbukumbu zake akilini mwa watu. Badala yake nitaweka siku ambayo haina ukubali wa Mungu, siku ambayo haiwezi kuwa ishara kati ya Mungu na watu wake. Nitawaongoza wale wanaoipokea siku hii na kuitakasa badala ya siku ya saba iliyobarikiwa na Mungu.Mar 162.2

    “Kupitia mwakilishi wangu duniani, nitajitukuza. Siku ya kwanza ya juma itaheshimika, na dunia ya Kiprotestanti itapokea Sabato bandia kama Sabato halisi. Kupitia kutoiheshimu Sabato iliyoanzishwa na Mungu, nitafanya sheria ya Mungu idharaulike. Maneno, “Iwe ishara kati yangu nanyi kwa vizazi vyote,” nitalazimisha yawe yanaelekezwa kwa Sabato yangu bandia.Mar 162.3

    “Hivyo ulimwengu utakuwa chini ya himaya yangu. Nitakuwa mtawala wa dunia, mkuu wa ulimwengu. Nitaongoza akili zilizo chini ya mamlaka yangu zisadiki kuwa Sabato ya Mungu ni jambo la kudharaulika. Ishara? Nitafanya ushikaji wa Sabato ya siku ya saba uwe ishara ya ukaidi dhidi ya mamlaka za dunia. Sheria za wanadamu zitakazwa ziwe kali mno kiasi kwamba wanadamu hawatadiriki kuitunza Sabato ya siku ya saba. Kwa hofu ya kukosa chakula na mavazi watajiunga na ulimwengu kuiasi sheria ya Mungu. Ulimwengu mzima utakuwa chini ya madaraka yangu.”Mar 162.4

    Sabato itakuwa kipimo kikuu cha utii, kwani ndilo eneo la ukweli linaloshindaniwa. Wakati majaribu makuu yaliyo mtihani wa mwisho yatakapowakabili wanadamu, ndipo mstari utachorwa kati ya wale wamtumikiao Mungu na wale wasiomtumikia.Mar 162.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents