Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Ushuhuda Unaohitajika Duniani, Sura ya 106

    Ninyi ndinyi barua yetu, iliyoandikwa mioyoni mwetu, inajulikana na kusomwa na watu wote. 2 Wakorintho 3:2.Mar 114.1

    Badiliko la tabia ni ushuhuda wa uwepo wa upendo wa Kristo kwa ulimwengu. Bwana anategemea watu wake waoneshe ya kwamba nguvu ya neema inayokomboa yaweza kufanya kazi katika kurekebisha tabia zilizo na makosa na kusababisha ziendelee katika mlingano na utoaji wa matunda usio wa kawaida.Mar 114.2

    Lakini ili tutimize makusudi ya Mungu, yapo maandalizi yapaswayo kufanywa. Bwana anatuhitaji tusafishe ubinafsi toka mioyoni mwetu, ambao ndiyo mzizi wa utengano. Nafsi inapokuwa imetolewa kwa Mungu, macho yetu yatafunguliwa ili kuona vikwazo ambavyo hali ya kutokuwa kwetu kama Kristo imeviweka katika njia ya wengine. Mungu anatuhitaji tuyaondoe yote haya. Anasema: “Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa.” Yak. 5:16. Ndipo tutakuwa na uhakika aliokuwa nao Daudi baada ya kuungama dhambi yake. Aliomba: “Unirudishie furaha ya wokovu wako; unitegemeze kwa roho ya wepesi. Nitawafundisha wakosaji njia zako, na wenye dhambi watarejea kwako.” Zab. 51:12,13.Mar 114.3

    Neema ya Mungu inapotawala ndani, roho itazingirwa na hali ya imani na ujasiri na upendo wa Kristo, hali ambayo hutia nguvu maisha ya kiroho kwa wote wanaoiruhusu iingie ndani yao... Kila mmoja ambaye ni mshirika wa upendo wa Kristo unaosamehe, kila mmoja ambaye ameangaziwa na Roho wa Mungu na kuongoka katika ukweli, kwa sababu ya baraka hizi pekee, atahisi kuwa na deni kwa ajili ya kila roho anayokutana nayo. Wale walio wanyenyekevu katika mioyo yao, Bwana atawatumia kufikia roho ambazo wachungaji waliowekewa mikono hawawezi kuzifikia. Wataongozwa kunena maneno yafunuayo neema ya Kristo inayookoa.Mar 114.4

    Vilevile, katika kubariki wengine wao wenyewe watabarikiwa. Mungu anatupatia fursa ya kuwasilisha neema, ili atujaze upya na kutuongezea neema zaidi. Tumaini na imani vitaimarika wakati wakala wa Mungu atendapo kazi akitumia talanta na nyenzo ambazo Mungu amezitoa. Atakuwa akitenda kazi na wakala wa kiungu .Mar 114.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents