Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Somo Kutoka Bethlehemu, Sura ya 2

    Kadhalika Kristo naye, akiisha kutolewa sadaka mara moja azichtikue dhambi za watu wengi, atatokea mara ya pili, pasipo dhambi, kwa hao wamtazaniao kwa wokovu. Waebrania 9:28.Mar 10.1

    Wakati wa ujio wa kwanza wa Kristo, makuhani na waandishi wa ule Mji Mtakatifu, ambao walikuwa wamepewa maagizo ya Mungu, wangeweza kuzitambua ishara za nyakati na kuutangaza ujio wa yule aliyekuwa ameahidiwa. Unabii wa Mika ulikuwa unataja mahali ambapo angezaliwa; Danieli alitaja muda wa kuja kwake. Mungu aliwakabidhi viongozi wa Wayahudi unabii huu; walikuwa hawana udhuru kwa kutokujua na kutotangaza kuwa ujio wa Yesu ulikuwa umekaribia. Kutokujua kwao kulikuwa kumesababishwa na uzembe ambao ni dhambi.Mar 10.2

    Watu wote walikuwa wanapaswa kukesha na kungoja ili wawe wa kwanza kumpokea Mkombozi wa ulimwengu. Lakini, tazama, kule Bethlehemu, wageni wawili kutoka katika milima ya Nazareti waliokuwa wamechoka, walikuwa wakizunguka mtaa mzima hadi mashariki kabisa mwa mji, wakitafuta mahali pa kupumzika na kujisetiri bila mafanikio. Hakuna milango iliyokuwa wazi kwa ajili ya kuwapokea. Hatimaye walijibanza katika banda moja chafu la kulala ng’ombe, na hapo ndipo Mwokozi wa ulimwengu alipozaliwa. . .Mar 10.3

    Hakukuwa na dalili zo zote kwamba Kristo alikuwa anatarajiwa kuja, na wala hakukuwa na maandalizi yo yote kwa ajili ya Mfalme wa uzima. Mjumbe kutoka mbinguni, akiwa amepigwa na butwaa, alitaka kurudi mbinguni akiwa na habari za aibu, ndipo alipoona kundi la wachunga kondoo waliokuwa wakilinda kondoo wao usiku, na walipokuwa wakitazama nyota za mbinguni, walikuwa wanatafakari unabii juu ya Masihi aliyekuwa akitarajiwa kuja duniani, huku wakiwa na hamu kubwa ya ujio wa Mkombozi wa ulimwengu. Hili lilikuwa kundi la watu ambao walikuwa tayari kuupokea ujumbe kutoka mbinguni. Na ghafla malaika wa Bwana alitokea, akitangaza habari njema za furaha kubwa. . .Mar 10.4

    Kisa hiki cha Bethlehemu ni somo zuri sana! Kinakemea kutoamini kwetu, kiburi chetu, na kujikinai kwetu. Kinatuonya ili tuwe na tahadhari tusije tukashindwa kuzitambua ishara za nyakati, na kutoujua wakati wa kujiliwa kwetu, kutokana na tabia yetu ya kutokujali.Mar 10.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents