Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Furaha Katika Utii, Sura ya 71

    Ee BWANA, nimeutamani wokovu wako, na sheria yako ndiyo furaha yangu. Zaburi 119:174.Mar 79.1

    Kamwe Mkristo wa kweli hatalalamika ya kwamba nira ya Kristo inachubua shingo yake. Atakuwa akidumu kuhesabu ya kwamba huduma yake kwa Yesu ni uhuru ulio kamili. Sheria ya Mungu ni furaha yake. Badala ya kutafuta kushusha hadhi ya amri za Mungu ili zipelekane na mapungufu yake, atadumu kupambana ili ainuke na kufikia kiwango cha ukamilifu. Huo unapaswa kuwa uzoefu wetu kama kweli tunataka kuwa tayari kusimama katika ile siku ya Mungu. Sasa, wakati rehema inapoendelea kuwepo, wakati sauti ya rehema inapoendelea kusikika, ni wasaa kwa ajili yetu kutupilia mbali dhambi zetu...Mar 79.2

    Mungu alitangulia kutuandalia kwa wingi kila tunachokihitaji ili tupate kusimama tukiwa wakamilifu katika neema yake, bila kupungukiwa na chochote, wakati tukisubiri ujio wa Bwana wetu. Je, uko tayari? Je, umevaa vazi la arusi? Kamwe vazi hilo halitaficha uongo, uchafu, ufisadi, au unafiki. Jicho la Mungu li juu yako.. tunaweza kuficha dhambi zetu machoni pa watu, lakini hatuwezi kuficha chochote mbele za Mwumbaji wetu.Mar 79.3

    Mungu hakuacha kumtoa Mwanawe wa pekee, bali alimkabidhi hata kwa mauti kwa ajili ya makosa yetu na kumfufua tena ili tufanywe kuwa wenye haki. Kupitia kwa Kristo tunaweza kuwasilisha maombi yetu kwenye kiti cha Neema. Kupitia kwake, hata ingawa hatustahili kama tulivyo, tunaweza kupata baraka zote za kiroho. Je, tunamjia Yeye, ili tupate uzima?Mar 79.4

    Mapenzi ya Mungu yanaelezwa katika maagizo ya sheria yake takatifu, na kanuni za sheria hii ni kanuni za mbinguni. Malaika wa mbinguni hawapambani kwa ajili ya ufahamu mwingine wowote ulio wa juu kuliko kujua mapenzi ya Mungu, na kutenda mapenzi yake ni huduma ya juu kuliko zote iwezayo kuchukua nguvu zao.Mar 79.5

    Lakini mbinguni, huduma haitolewi katika misingi ya kutimiza sheria. Wakati Shetani alipoasi dhidi ya sheria ya Yehova, wazo la uwepo wa sheria liliwajia malaika kama uamsho kwa suala ambalo hawakuwa wamepata kuliwazia kabla. Katika huduma malaika hawapo kama watumishi, bali kama wana... Kwao utii siyo kazi ngumu. Upendo wao kwa Mungu hufanya huduma yao kuwa ya furaha. Kwa hiyo ndani ya kila roho ambapo Kristo anaishi, yeye aliye tumaini la utukufu, maneno yake yanasikika kama mwangwi tena, “Ee BWANA, nimeutamani wokovu wako, na sheria yako ndiyo furaha yangu.”Mar 79.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents