Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Wasaa wa Kuamua!, Sura ya 100

    Chagueni hivi leo mtakayemtumikia. Yoshua 24:15Mar 108.1

    Leo, dunia imekuwa kichaa: hali ya kuchanganyikiwa imo kwa waume kwa wake, na inawaendesha kasi kuelekea katika uharibifu. Kila aina ya mazoea mabaya inatawala, na watu wamepumbazwa na uovu kwa kiasi kikubwa hata kutoweza kusikiliza maonyo na miito.Mar 108.2

    Bwana anasema kwa wote duniani,“Chagueni hivi leo mtakayemtumikia.” Wote wamo katika kufanya maamuzi kwa ajili ya hatima yao ya milele. Watu wanapaswa kuamshwa watambue uzito wa wakati uliopo na ukaribu wa siku rehema itakapofikia mwisho. Mungu hamwambii mwanadamu ya kwamba bado miaka mitano, au kumi au ishirini hadi kufungwa kwa historia ya dunia hii. Hawezi kutupa mtu kisingizio chochote ili acheleweshe maandalizi ya kumlaki ajapo. Hatampa mtu sababu ya kusema kama yule mtumwa mbaya, “Bwana wangu anakawia kuja;” kwani hili linapelekea mtu kuzembea katika nafasi na fursa alizopewa ili kujiandaa kwa ajili ya siku ile kuu.Mar 108.3

    Kila mmoja anayedai kuwa mtumishi wa Mungu anaitwa kuhudumu kwa ajili yake kila siku kana kwamba ni siku yake ya mwisho...Mar 108.4

    Hebu tafakari juu ya kuja upesi kwa Mwana wa Adamu katika mawingu ya mbinguni akiwa na mamlaka na utukufu mkubwa. Usiiahirishe siku hiyo mawazoni mwako. . .Mar 108.5

    Hapa ndipo ulipo mzigo mkubwa wa kubebwa na kila mtu. Je, dhambi zangu zimesamehewa? Je, Kristo anayebeba mzigo wa dhambi, ameichukua hatia yangu? Je, mimi ninao moyo safi, uliosafishwa na haki ya Yesu Kristo? Ole wa roho ile isiyotamtafuta Kristo kama kimbilio. Ole wao wote ambao kwa namna yoyote wanatoa mawazo toka katika kazi, na kusababisha udhaifu wa roho yoyote wakali huu. . .Mar 108.6

    Kazi iliyo kuu kwa sasa ambayo mawazo yetu hayapaswi kutoka kwayo ni tafakuri ya msimamo wa mtu binafsi mbele za Mungu. Je, miguu yetu ipo katika Mwamba wa Kale? Je, tumejificha katika Yeye aliye Kimbilio pekee? Dhoruba inakuja, isiyo na huruma kwa ghadhabu yake. Je, tumejiandaa kukabiliana nayo? Je, tu kitu kimoja pamoja na Kristo kama jinsi Yeye alivyo mmoja na Baba? Je, sisi ni warithi wa Mungu na pia warithi pamoja na Kristo?. . .Mar 108.7

    Tabia ya Kristo inapaswa kuwa tabia yetu. Tunapaswa kubadilishwa kwa kugeuzwa nia zetu. Hapa ndipo ulipo usalama wetu. Hakuna kiwezacho kutengenisha Mkristo aliye hai na Mungu.Mar 108.8

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents