Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Uzoefu Hai na wa Kina, Sura ya 89

  Sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Waebrania 2:3.Mar 97.1

  Niliona ya kwamba hatupaswi kuahirisha suala la ujio wa Bwana. Malaika alisema: “Jiandaeni, jiandaeni, kwa ajili ya kile kinachokuja duniani. Hebu kazi zenu zipelekane na imani yenu. “Niliona ya kwamba mawazo yanapaswa kuwekwa kwa Mungu, na mvuto wetu unapaswa kumshuhudia Mungu na kweli yake. Hatuwezi kumheshimu Bwana hali tukiwa wazembe na tusiojali... Tunapaswa kuwa makini katika kuthibitisha wokovu wa roho zetu wenyewe, na pia kwa ajili ya kuwaokoa wengine. Tunapaswa kulipatia jambo hili umuhimu wote, na mengine yote yatafuatia.Mar 97.2

  Niliona uzuri wa mbinguni. Nilisikia malaika wakiimba nyimbo za furaha, wakiimba sita, heshima, na utukufu kwa Yesu. Kisha nikatambua kitu kuhusu upendo wa ajabu wa Mwana wa Mungu. Aliuacha utukufu wote, heshima yote aliyokuwa nayo mbinguni, na alipendezwa sana na wokovu wetu kiasi cha kuwa mnyenyekevu katika kujitwika kwa uvumilivu kila namna ya ufidhuli na dharau ambayo mwanadamu alimtupia. Alijeruhiwa, akapigwa, na kuumizwa; alitundikwa katika msalaba wa Kalvari na kufa kwa maumivu makali zaidi ili kutuokoa na mauti, ili tupate kuoshwa katika damu yake na tufufuliwe kuishi pamoja naye katika makao anayotuandalia, ili tufurahie nuru na utukufu wa mbinguni, kusikia malaika wanapoimba, na hata kuimba pamoja nao.Mar 97.3

  Niliona ya kuwa mbingu yote inapendezwa na wokovu wetu; na je, sisi tusijali? Je, sisi tutakuwa wazembe, kana kwamba suala la wokovu wetu ni jambo dogo? Je, tutadharau kafara ambayo imetolewa kwa ajili yetu?Mar 97.4

  Tumepewa Kitabu ili kiongoze miguu yetu inapopita katika hatari za ulimwengu huu wenye giza na kuingia mbinguni. Kinatuambia jinsi tuwezavyo kuepuka ghadhabu ya Mungu na pia kinatuambia juu ya mateso ya Kristo kwa ajili yetu, kafara iliyo kuu ambayo imetolewa ili tupate kuokolewa na kufurahia uwepo wa Mungu milele.Mar 97.5

  Mfano wa litatiwa hautamwokoa yeyote. Wote wanapaswa kuwa na uzoefu wa ndani kabisa na ulio hai. Hii ndiyo njia pekee ya kuwaokoa wakati wa taabu. Kisha kazi zao zitapimwa kwa jinsi zilivyo; na kama zipo kama dhahabu, fedha, au vito vya thamani zitafichwa sirini mwa hema la Bwana.Mar 97.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents