Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Mwelekeo Mmoja tu Ulio Salama, Sura ya 49

  Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu. Mathayo 26:41Mar 57.1

  Nisemeje basi ili kuamsha watu wa Mungu waliosalia?.. .Ninawaonya wote wajiitao kwa jina la Kristo ili wajichunguze wenyewe kwa makini na kufanya maungamo ya kina kwa ajili ya makosa yao yote, ili wayatangulize hukumuni, na pia hili lipelekee malaika anayetunza taarifa kuandika “msamaha” mbele ya majina yao. Kaka yangu, dada yangu, kama nyakati nzuri za rehema hazikutumiwa ipasavyo, utaachwa ukiwa huna udhuru. Kama hujitahidi kwa namna yoyote kuamka, kama huwi na azma ya kutubu, nyakati hizi za pekee zitapita kwa haraka, na utapimwa kwenye mizani na kukutwa umepungua.Mar 57.2

  Yesu anapoonya “kesheni mkisali,” anaonesha mwelekeo pekee ulio salama. Lipo hitaji la kukesha. Mioyo yetu wenyewe ni midanganyifu; tumezingwa na udhaifu na kasoro za kibinadamu, na kusudio la Shetani ni kuangamiza. Twaweza kutokuwa macho tu kwa muda mfupi, lakini adui yetu kamwe haachi kufanya kazi. Kwa sababu tunajua anavyojitahidi bila kuchoka, na tusilale, kama wengine, bali “tukeshe na tuwe macho.” Ni lazima tukutane na mvuto na mtazamo wa ulimwengu huu, lakini sharti hivi visiruhusiwe kutawala mawazo na moyo.Mar 57.3

  Kwa karibu sana, hebu uchunguze moyo wako mwenyewe katika nuru ya umilele. Usifiche chochote katika uchunguzi huu. Chunguza, naam, chunguza kama utafutaye uhai wako, na ujihukumu mwenyewe, jitamkie hatma yako mwenyewe, na halafu kwa imani dai damu itakasayo ya Kristo ili iondoe madoa toka katika tabia yako ya Kikristo. Usijiliwaze au kujipatia udhuru. Shughulika kikweli kweli na roho yako mwenyewe. Kisha pale unapojiona kamam mwenye dhambi, anguka ukiwa umevunjika chini ya msalaba. Yesu atakupokea, vivyo hivyo ukiwa umechafuka, kisha atakuosha katika damu yake, na kukusafisha toka katika udhalimu wote, na kukufanya ufae katika jamii ya malaika mbinguni, katika mbingu iliyo safi na yenye amani. Hakuna mkwaruzo, hakuna ukengeufu pale. Ni afya tele, furaha na amani.Mar 57.4

  Ulimwengu huu ni shule ya mafunzo inayoandaa kwa ajili ya shule ya juu, maisha haya ni kwa ajili ya maandalizi kwa ajili ya maisha yajayo. Hapa tunapaswa kujiandaa kwa ajili ya kuingia kwenye kumbi za mbinguni. Hapa tunapaswa kupokea na kuamini na kufanyia mazoezi ukweli hadi tutakapofanywa tayari pamoja na watakatifu walio nuruni kwa ajili ya kuwa nyumbani.Mar 57.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents