Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Afya ya Kimwili na Fikra Adilifu, Sura ya 73

  Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho. 1 Petro 2:11.Mar 81.1

  Wengi wanalifikiria fungu hili kama linalokemea uasherati tu; lakini lina maana iliyo pana zaidi. Linakemea kila namna ya kujifurahisha katika vyakula na tamaa zinazoharibu. Kila namna ya hamu iliyo potofu huwa tamaa ifanyayo vita dhidi ya mwili. Tulipewa hamu ya chakula kwa makusudi mazuri, haikukusudiwa iwe mjumbe wa mauti kutokana na upotofu, na matokeo yake, kudhalilika hadi kuwa “tamaa za mwili zipinganazo na roho.” Petro anapoasa anatoa onyo kali lililo wazi na la moja kwa moja dhidi ya matumizi yote ya vichocheo na madawa ya kulevya. Kuendekeza haya kunapelekea katika kiwango cha tamaa ambazo huwa zinaweka mvuto unaoumiza kwa maisha ya mtu kimaadili.Mar 81.2

  Hebu yeyote anayedai kuwa mtauwa asipuuzie afya ya mwili, huku akijidanganya mwenyewe ya kwamba kutokuwa na kiasi siyo dhambi na kwamba hilo halitaathiri hali yao ya kiroho. Yapo mahusiano ya karibu sana kati ya mwili na maadili. Kiwango cha maadili kitainuliwa ama kushushwa kutokana na mazoea ya kimwili. Kama chakula si kizuri sana kiafya, madhara yake yatakuwa makubwa zaidi. Mazoea yoyote ambayo hayahamasishi utendaji kiafya ndani ya mfumo wa kibinadamu yanahafifisha akili iliyopaswa kuwa ya kiungwana ...Uendekezaji wa uchu wa kula huwa unaimarisha tabia za kinyama, na kuziwezesha kukua kuliko nguvu za kiakili na kiroho.Mar 81.3

  Nguvu ya jaribu la kuendekeza uchu wa chakula laweza kupimwa tu kwa maumivu makali yasiyoelezeka ya Mkombozi wetu katika saumu ile ndefu pale jangwani. Alijua ya kwamba uendekezaji potofu wa hamu ya chakula ungeua mtazamo wa mtu kiasi cha kutoweza kuelewa mambo matakatifu. Kama uwezo au nguvu ya hamu ya chakula ulikuwa na nguvu hivi kwa wanadamu, kiasi ambacho ilimpasa Mwana wa Mungu aje kuvunja nguvu yake kwa niaba ya mwanadamu, akifunga takriban kwa majuma sita, basi kazi iliyo mbele ya Mkristo ni kubwa kuliko kawaida! Hata hivyo, hata kama mapambano ni makubwa kiasi gani, anaweza kushinda. Kwa msaada wa uweza wa kimbingu ambao ulishinda dhidi ya majaribu makali kuliko yote ambayo Shetani amepata kuyavumbua, yeye pia, anaweza kushinda kikamilifu katika vita yake hii dhidi ya uovu, na hatimaye aweza kuvaa taji ya mshindi katika ufalme wa Mungu.Mar 81.4

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents