Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Kipaumbele cha Juu Kabisa cha Maisha, Sura ya 63

    Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. Mathayo 6:33Mar 71.1

    Ufalme wa mbinguni, haki ya Kristo ndilo kusudi la kwanza lililo kuu. Makusudi mengine yote yanapaswa kuwa ya pili baada ya hili.Mar 71.2

    Shetani ataiwasilisha njia ya utauwa kama iliyo ngumu wakati njia za anasa za kidunia zikionekana kupambwa kwa maua. Kwa kutumia rangi za uongo na zilizopendezeshwa mjaribu atauvisha ulimwengu na anasa mbele yenu. Kiburi ni moja ya tabia zenye nguvu sana katika asili yetu iliyoharibika, na anajua ya kwamba anaweza kuitumia hiyo kwa namna yenye mafanikio makubwa. Atakudanganya kupitia kwa mawakala wake. Utapokea sifa ambazo zitainua majivuno yako na kupalilia kiburi chako na hali ya kujiona, na waweza kudhani ya kwamba ukiwa na faida za namna hiyo pamoja na mivuto ni jambo la huzuni kabisa kwako kutoka na kujitenga na dunia na kuwa Mkristo....Lakini tafakari haya; ya kwamba anasa za dunia zitakuwa na mwisho, na kile upandacho ndicho utakachovuna. Je, mivuto binafsi, uwezo au talanta ni vya thamani mno kiasi ambacho haviwezi kukabidhiwa kwa Mungu, aliye chanzo cha uwepo wako, Yeye akulindaye kila wakati? Je, uwezo wako una thamani kwako sana kiasi ambacho huwezi kuukabidhi kwa Mungu?Mar 71.3

    Vijana husisitiza ya kwamba wanahitaji kitu kuamsha mawazo yao na kuyaelekeza katika maeneo mapya. Niliona ya kwamba kuna furaha katika kufanya kazi, ridhaa katika utumishi wenye manufaa. Hata hivyo, bado wengine husisitiza ya kwamba lazima kuwa na kitu fulani. . . ambacho kwacho mawazo huelekezwa kwa ajili ya tulizo au burudani wakati wa mahangaiko na kusota katika kazi. Tumaini la Kikristo ndilo lililo hitaji. Dini itakuwa mfariji wa kweli kwa muumini, kiongozi hakika ipelekayo katika chemchemi ya furaha ya kweli. Walio vijana wanapaswa kujifunza neno la Mungu na kujitoa nafsi zao katika kutafakari na kusali, na watatambua ya kwamba muda wao wa ziada umetumika vizuri sana.Mar 71.4

    Rafiki zangu vijana, munapaswa kutumia wakati kujihakikisha ninyi wenyewe, kama kweli mumo katika upendo wa Mungu. Jitahidini kufanya uchaguzi na wito wenu kuwa wa hakika.Mar 71.5

    Tafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake. Fanyeni hili kuwa la kwanza na la mwisho. Tafuteni kwanza kwa dhati kumjua yeye ambaye katika kumjua ilivyo sahihi mnapata uzima wa milele. Wokovu wa roho ni Kristo na haki yake.Mar 71.6

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents