Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Sanamu ya Mnyama Kusimikwa, Sura ya 156

  “Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile aliyopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga naye akaishi.” Ufunuo 13:14.Mar 164.1

  Sanamu ya mnyama itaundwa kabla ya kufungwa kwa mlango wa rehema; kwani itakuwa ndiyo mtihani mkuu kwa watu wa Mungu, ambao kwa huo mustakabali wao wa umilele utaamuliwa....Mar 164.2

  Katika Ufunuo 13 somo hilo limeelezewa kwa kinagaubaga: “Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa MwanaKondoo, akanena kama joka. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona.” (aya ya 11,12). Kisha mamlaka hii itendayo miujiza inafunuliwa: “Naye awakosesha wale wakaao juu ya nchi, kwa ishara zile alizopewa kuzifanya mbele ya huyo mnyama, akiwaambia wakaao juu ya nchi kumfanyia sanamu yule mnyama, aliyekuwa na jeraha la upanga, naye akaishi. Akapewa kutia pumzi katika ile sanamu ya mnyama, hata ile sanamu ya mnyama inene, na kuwafanya hao wote wasioisujudu sanamu ya mnyama wauawe. Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao: tena kwamba mtu awaye yote asiweze kununua wala kuuza, isipokuwa ana chapa ile, yaani, jina la mnyama yule, na hesabu ya jina lake.” (aya 14-17)Mar 164.3

  Huu ni mtihani ambao watu wa Mungu wataupitia kabla ya kuwekwa muhuri. Wote walio waaminifu kwa Mungu wakiitii sheria yake, na kuikataa sabato bandia, watakuwa chini ya bendera ya Yehova Bwana Mungu, nao watapokea muhuri wa Mungu aliye hai. Wale ambao hupuuzia ukweli wa kimbingu, na kukumbatia ibada ya jumapili, watapokea alama ya mnyama. . . .Mar 164.4

  Wakati Yohana alipooneshwa matatizo makuu yatakayolikabili kanisa mnamo siku za mwisho dhidi ya mamlaka za dunia, aliruhusiwa kuona ushindi mkuu na ukombozi wa waaminifu. . . . Akitazama ng’ambo ya moshi na ghasia za pambano, aliona kundi zuri katika mlima Sayuni likiwa pamoja na MwanaKondoo, badala ya kupokea alama ya mnyama, wao “wanalo jina la Baba limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.”Mar 164.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents