Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Kutiwa Nguvu na Upendo, Sura ya 93

  Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake. 1 Yohana 4:21.Mar 101.1

  Upendo ni msingi, wa utauwa. Hata mtu awe bingwa katika fani gani, hakuna mtu mwenye upendo ulio safi kwa Mungu kama hampendi nduguye kwa moyo mweupe. . . Wakati nafsi iunganishwapo katika Kristo, upendo huchipuka wenyewe. Ukamilifu wa tabia ya Kikristo hupatikana wakati msukumo kwa ajili ya kusaidia na kubariki wengine unapotokea ndani ya moyo kwa kudumu- wakati mwanga wa jua la mbinguni unapojaza moyo na hivyo kufunuliwa katika mwonekano. . .Mar 101.2

  Tukiungana na Kristo, tunakuwa tumeunganishwa na watu wengine kwa mnyororo wa upendo. Kisha huruma na rehema za Kristo zitadhihirika katika maisha yetu. Hatutasubiri hadi wahitaji na wenye shida waletwe kwetu. Haitakuwa lazima mtu atusihi ili tuwahurumie wenye matatizo. Itakuwa ni asili yetu kuhudumu kwa ajili ya wahitaji na wanaoteseka kama ilivyokuwa kwa Kristo aliyekuwa akizunguka hali akitenda mema....Mar 101.3

  Utukufu wa Mungu upo katika kuwainua walioanguka, kufariji waliosetwa. . . Misingi ya utaifa, rangi, au ukoo haumfanyi mtu kuonekana wa pekee kwa Mungu. . . Watu wote ni wa familia moja kutokana na uumbaji, na wote ni wamoja kupitia katika ukombozi. Kristo alikuja ili kubomoa kuta zilizogawa watu, kufungua wazi malango ya hekalu, ili kila roho iwe na uhuru kumfikia Mungu. Upendo wake ni mpana sana, wenye kina sana, uliojaa, kiasi ambacho waweza kupenya popote. Huinua toka kwa himaya ya Shetani roho dhaifu ambazo zimezongwa na udanganyifu. Upendo huu huwaweka watu karibu kabisa na kiti cha enzi cha Mungu, ambacho kimezingwa na upinde wa ahadi. . .Mar 101.4

  Kristo anatafuta kuwainua wote ambao wameinuliwa na urafiki wake, ili tuwe kitu kimoja naye kama yeye alivyo na Baba yake. Anaturuhusu tukutane na mateso na maafa ili kutuita tutoke katika ubinafsi; anatafuta kuendeleza ndani yetu silika za tabia yake - rehema, wema na upendo. . .Mar 101.5

  “Kama ukienda katika njia zangu,” Bwana asema, “nitakupa nafasi ya kumkaribia kati yao wasimamao karibu.”- hata kati ya malaika waokizunguka kiti chake cha enzi (Zek. 3:7.) Kwa kushirikiana na walio mbinguni katika kazi yao duniani, tunajiandaa kwa ajili ya kuwa pamoja nao mbinguni.Mar 101.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents