Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Atatawala Milele, Sura ya 13

  Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele. Ufunuo 11:15.Mar 21.1

  Ujio wa Kristo kuja kuanzisha ufalme wa haki umekuwa ukichochea kauIi za kusisimua sana kutoka kwa waandishi wa Maandiko Matakatifu.... Mwandishi wa Zaburi aliimba juu ya uwezo wa Mungu na utukufu wa mfalme wa Israeli: ... “Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie mbele za Bwana kwa maana anakuja, kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, na mataifa kwa uaminifu wake, Zab. 96:11-13.Mar 21.2

  Nabii Isaya alisema:... “Amemeza mauti hata milele: na Bwana Mungu atafuta machozi katika nyuso zote: na aibu ya watu wake ataiondoa katika ulimwegu wote: Maana Bwana amesema hayo. . . Isaya 25:8Mar 21.3

  Wakati Mwokozi alipokuwa anakaribia kuondolewa kutoka kwa wanafunzi wake, aliwafariji walipokuwa katika majonzi kwa kuwahakikishia kuwa angekuja tena: “Msifadhaike mioyoni mwenu: . . . Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi:... ninakwenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu.” Yn. 14:1-3.Mar 21.4

  Malaika waliobaki kwenye mlima wa mizeituni baada ya Yesu kupaa waliirudia ahadi hiyo ya kurudi kwa Yesu: “Huyu Yesu aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda juu mbinguni, atakuja jinsi iyo hiyo mliyomwona akienda zake mbinguni.” Mdo. 1:11. Naye mtume Paulo, akinena kwa uvuvio wa Roho, alishuhudia akisema, “Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu.” 1 The.4:16. Nabii aliyekuwa katika kisiwa cha Patmo anasema; “Tazama yuaja na mawingu, na kila jicho litamwona.” Ufu. 1:7.Mar 21.5

  Kuja kwake kutazungukwa na utukufu ule wa “zamani za kufanya upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa vinywa vya manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu.” Mdo. 3:21. Kisha utawala wa uovu uliodumu kwa muda mrefu utavunjwa; “falme za dunia hii” zitakuwa “ufalme wa Bwana wetu, na wa Kristo wake; naye atatawala milele hata milele.” Ufu. 11:15.Mar 21.6

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents