Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
  • Results
  • Related
  • Featured
No results found for: "".
  • Weighted Relevancy
  • Content Sequence
  • Relevancy
  • Earliest First
  • Latest First
    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents

    Pigeni Kelele !, Sura ya 98

    Pigeni tarumbeta katika Sayuni, pigeni na kelele katika mlima wangu mtakatifu; wenyeji wote wa nchi na watetemeke; kwa maana siku ya BWANA inakuja. Yoeli 2:1Mar 106.1

    Mambo yahusuyo mahitaji yetu ya milele yanapaswa sasa kutawala mawazo yetu. Hatuwezi kuyapa mambo ya kimbingu nafasi ya pili... Tunazo hukumu za Mungu, Zinatoa onyo la dhati kabisa zikisema; “mwe tayari; kwa maana saa msiyoijua Mwana wa Adamu yuaja.”Mar 106.2

    Wapo wengi, wengi sana makanisani mwetu wanaojua kidogo sana maana halisi ya ukweli wa wakati huu. Natoa wito kwao wasidharau utimilifu wa dalili za nyakati, zinazoonesha wazi kabisa ya kwamba mwisho umekaribia. Ni wengi sana ambao hawajatafuta wokovu wa roho zao ambao watatoa kilio hiki cha kusikitisha; “Mavuno yamepita, wakati wa hari umekwisha, wala sisi hatukuokoka”!Mar 106.3

    Tumo katikati ya matukio yafungavo historia ya dunia hii. Unabii unatimia kwa kasi. Saa ya rehema yanapita upesi. Hatuna muda - hatuna wasaa wa kupoteza. Hebu tusikutwe tumelala katika zamu zetu. Hebu asiwepo atakayesema moyoni mwake au katika matendo yake, “Bwana wangu anachelewa kuja.” Hebu ujumbe wa marejeo ya Kristo hivi karibuni utoe onyo kwa maneno yaliyo dhahiri. Hebu mshawishi waume kwa wake kila mahali watubu, na waikimbie ghadhabu inayokuja. Tuwaamshe wapate kufanya maandalizi mara moja; kwani hatujui zaidi juu ya kile kitakachofuata. Wachungaji na walei na waende katika mashamba yenye mazao yaliyoiva tayari..Mar 106.4

    Bwana anakuja upesi, na tunapaswa kukutana naye kwa amani. Na tukusudie kutenda yote kulingana na uwezo wetu kuweka nuru kwa wale wanaotuzunguka. Hatupaswi kuwa na huzuni, bali kuchangamka, na tunapaswa kuwa na Bwana wetu Yesu daima mbele zetu... Tunapaswa kuwa tayari na kusubiri ujio wake. Kumuona Yeye na pia kukaribishwa kama waliokombolewa kutakuwa na utukufu wa kushangaza! Tumesubiri kwa muda mrefu, lakini imani yetu haipaswi kudhoofika. Tutakapomwona Mfalme katika uzuri wake, tutabarikiwa milele na milele. Nahisi nataka kupiga kelele na kusema, “Tunaingia nyumbani!” Tumekaribia wakati ambapo Kristo atakuja kwa nguvu na utukufu mwingi, kuchukua waliokombolewa hadi katika nyumba yao ya milele.Mar 106.5

    Larger font
    Smaller font
    Copy
    Print
    Contents