Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Ukengeufu Wafungua Njia, Sura ya 157

  “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu” 2 Wathesalonike 2:3.Mar 165.1

  Wakati kanisa la awali lilipokuwa limenajisika kwa kutanga mbali kutoka kwa usahili wa injili Wakapokea taratibu na desturi za kipagani, liIipoteza mvuto wa Roho na nguvu za Mungu; na ili kutawala dhamiri za watu, kanisa lilitafuta msaada wa nguvu za kisiasa. Matokeo yake yalikuwa upapa, kanisa ambalo lilitawala mamlaka ya serikali na kuyatumia kwa kutimiza malengo yake, hasa katika kuwaadhibu “wazushi.”. . .Mar 165.2

  Kila fursa ilipojitokeza ya kanisa kumiliki nguvu za kisiasa, alizitumia kuangamiza wapinzani wa mafundisho yake. Makanisa ya Kiprotestanti ambayo yamefuata nyayo za Rumi kwa kufanya mwafaka na mamlaka za kidunia wamedhihirisha shauku ya aina iyo hiyo ya kuzuia uhuru wa dhamiri. Kielelezo cha hayo kimefunuliwa kupitia mateso ya muda mrefu dhidi ya waasi wa kanisa la Uingereza. Mnamo karne ya kumi na sita na kumi na saba, maelfu ya wachungaji wasiolegeza msimamo walilazimika kutoroka makanisa yao, na wengi wakiwemo wachungaji na watu, walitozwa faini, walitupwa gerezani na kufa kama wafia dini.Mar 165.3

  Ilikuwa ni uasi ulioongoza kanisa la awali kutafuta msaada wa serikali za kiraia, na hii ilifungua njia kwa ukuaji wa Upapa—mnyama. Paulo anasema: “Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu.” 2 The 2:3. Hivyo uasi kanisani utafungua njia kwa ajili ya sanamu ya mnyama.Mar 165.4

  Shetani atatenda kazi kwa nguvu zote na “madanganyo yote ya udhalimu.” 2 The. 2:9, 10. Utendaji wake umedhihirika kwa uongezekaji uovu, wingi wa ukengeufu, uzushi na madanganyo ya siku hizi za mwisho. Siyo tu kwamba Shetani anauchukua ulimwengu mateka, ila ulaghai wake Unaleta chachu kwa makanisa yanayomkiri Bwana wetu Yesu Kristo. Uasi utakua hadi kuwa giza nene la usiku wa manane. Kwa watu wa Mungu utakuwa usiku wa majaribu, usiku wa maombolezo, usiku wa mateso kwa ajili ya ile kweli. lla kutoka kwa usiku huo wa giza nuru ya Mungu itachomoza.Mar 165.5

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents