Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Lengo Lipaswalo Kufikiwa, Sura ya 54

  Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo. 1 Wathesalonike 5:23Mar 62.1

  Wakati Paulo alipoandika, na “Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa,” hakuwa anawasihi nduguze kuazimia kufikia kiwango ambacho haikuwezekana kukifikia; hakuomba ya kwamba wapate mibaraka ambayo haikuwemo katika mapenzi ya Mungu. Alijua ya kwamba wote ambao wangestahili kukutana na Kristo kwa amani, sharti wawe na tabia iliyo takatifu na safi.Mar 62.2

  Kama Waadventista wa Sabato wangeishi kulingana na kile wanachodai kukiamini, kama wangekuwa wanamatengenezo wa kweli katika afya, ni hakika wangekuwa kivutio kwa ulimwengu, malaika na watu. Wangeonesha ari kubwa kwa ajili ya wokovu wa wale wasioujua ukweli.Mar 62.3

  Matengenezo makuu yapaswa kuonekana kati ya watu wanaodai kutazamia ujio wa Kristo ulio karibu. Matengenezo katika afya yanapaswa yafanye kazi ndani ya watu ambayo haijafanyika bado. Wapo wale ambao wanapaswa kuamka toka katika hatari ya kula nyama, ambao bado hula minofu, huku wakihatarisha afya kimwili, kiakili na kiroho.Mar 62.4

  Wengi ambao leo wameongoka nusu nusu tu katika suala la ulaji wa nyama wataachana na watu wa Mungu, kwa kwenda mbali nao.Mar 62.5

  Kutawaliwa na nguvu ya kupenda kula kutapelekea uharibifu wa maelfu, ambao, kama wangeshinda hilo wakati huu, wangekuwa na uwezo mkubwa kimaadili kuupata ushindi katika kila jaribu liletwalo na Shetani. Lakini wale walio watumwa wa kula watashindwa katika kukamilisha makosa ya tabia ya Kikristo. Mwendelezo wa makosa ya watu kwa miaka elfu sita umezaa matunda ya maradhi, maumivu na mauti. Na jinsi tunavyokaribia mwisho wa wakati, jaribu la Shetani la kuzamisha watu katika hamu ya kula litakuwa na nguvu zaidi na litakuwa gumu kulishinda.Mar 62.6

  Tena na tena nimeoneshwa ya kwamba Mungu anajaribu kutuongoza turejee hatua kwa hatua kwa mpango wake wa awali -ya kwamba mtu atumie viumbe vya asili vinavyomea duniani kwa chakula. Hatimaye ulaji wa nyama utaachwa kati ya wale wanaosubiri ujio wa Bwana; nyama itakoma kuwa sehemu ya lisle yao. Tunapaswa daima tuutazame mwisho huo, na tuwe radhi kulifanyia kazi hili bila kukoma.Mar 62.7

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents