Loading...
Larger font
Smaller font
Copy
Print
Contents

Maranatha

 - Contents
 • Results
 • Related
 • Featured
No results found for: "".
 • Weighted Relevancy
 • Content Sequence
 • Relevancy
 • Earliest First
 • Latest First
  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents

  Someni Danieli na Ufunuo., Sura ya 22

  Heri asomaye na wao wayasikiayo maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu. Ufunuo 1:3.Mar 30.1

  Ujumbe utakaoyaamsha makanisa unapaswa kutangazwa. Kila juhudi ifanywe kutoa nuru, si kwa watu wetu tu, lakini kwa ulimwengu. Nimeagizwa kwamba unabii wa Danieli na Ufunuo unapaswa kuandikwa katika vijitabu vidogo, vikiwa na ufafanuzi unaotakiwa, na unapaswa kupelekwa ulimwenguni kote. Watu wetu wenyewe wanapaswa kupatiwa nuru hii kwa namna iliyo wazi zaidi.Mar 30.2

  Wale wanaoula mwili na kunywa damu ya Mwana wa Mungu wataleta kutoka katika vitabu vya Danieli na Ufunuo ukweli uliovuviwa na Roho Mtakatifu. Wataanza kama vikosi maalum ambavyo havitaweza kutwezwa. Vinywa vya watoto vitafunguka na kutangaza siri ambazo zilikuwa zimefichwa kwa watu. . .Mar 30.3

  Hivi karibuni sehemu kubwa ya unabiii itatimizwa kwa mfululizo na kwa haraka. Kila kipengele cha nguvu kitatumika. Historia iliyopita itajirudia; migogoro ya kale itainuka upya, na hatari itawakabili watu wa Mungu kila upande. Fadhaa inaishika jamii ya wanadamu. Imeenea kila mahali katika dunia. . .Mar 30.4

  Someni Ufunuo sambamba na kitabu cha Danieli, kwani historia itajirudia. . . Sisi, tukiwa na fursa zote za kidini tulizo nazo, tunapaswa kujua mengi zaidi kuliko tunavyojua sasa.Mar 30.5

  Malaika wanatamani kuuona ukweli ambao umefunuliwa kwa watu ambao wanalichunguza Neno la Mungu kwa moyo wa toba na kuomba ili wapate kwa upana, urefu, kina, na kimo cha ufahamu ambao Yeye pake yake anaweza kuutoa.Mar 30.6

  Tunapokaribia mwisho wa historia ya ulimwengu huu, tunahitaji kuusoma unabii unaohusu siku za mwisho. Kitabu cha mwisho katika Agano Jipya kimejaa ukweli tunaotakiwa kuulewa. Shetani amepofusha akili za wengi kiasi kwamba wamefurahia udhuru wo wote ule wa kutokifanya kitabu cha Ufunuo kuwa somo lao la kila siku. Lakini Kristo, kwa njia ya mtumishi wake Yohana, ametueleza hapa mambo yatakayokuwa katika siku za mwisho; na anasema, “Heri asomaye na wao wayasikiayo maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo” Ufu. 1:3.Mar 30.7

  Larger font
  Smaller font
  Copy
  Print
  Contents